Baada ya Tz kuongoza kwa kua na uwekezaji mkubwa kutoka nje wa moja kwa moja yaani foreign direct investment, kwa kifupi FDI.
Wengine wameonekana kuponda nafasi mpya na endelevu ya Tz kama kiongozi kwenye mambo ya uchumi afrika mashariki, hawaamini, wanataka Tz iwe ya mwisho ili waseme sio unaona Tz hamna kitu, inasikitisha kwamba hawa ni wa Tz, wanasema wanavumilia kuwa waTz.
Lakini pia imeonekana wengi hawa fahamu maana hasa ya FDI, hatua gani zinafanya FDI iongezeke, na mazuri na yasiyo mazuri ya FDI.
Kutofahamu huko kunaleta kutoelewa kwa mikakati chanya na hatua endelevu zinazochukuliwa ili kuziongeza, ambapo matokeo yake ni kukua kwa uchumi, na kupunguza umasikini.
Mfano wa FDI kutoka nje kuja Tz ni kama kampuni za simu yaani VODACOM, Airtel, na Tigo. Nimetumia mfano huu kutokana na kwamba ni jambo ama mfano uliokua wazi kwa wengi, na mazuri yake yako wazi kwa kila mmoja. Mfano mwingine ni wa Bank ya CRDB kufungua matawi Burundi, ama Azam (Bakhressa group) kufungua matawi Malawi, mfano huu wa pili unaunyesha FDI kutokea Tz kwenda nchi nyingine. Kwamba sio wageni tu wanaowekeza Tz, bali hata waTz wanawekeza nje na hivyo kuwa FDI kwa nchi hiyo.
Kwanini nchi zinafanya jitihada kupata FDI, Tz ikiwa moja ya hizo nchi zinazofanya jitahada hizi za kuongeza FDI.
FDI zinasakwa kutokana na mitaji ya ndani kutotosha kukuza uchumi wa nchi, na hivyo kupata mitaji, na uwekezaji kutoka nje kuna ongezea mambo kama miundo mbinu, ajira, upatikanaji wa mikopo, uwepo ama kuja kwa technologia mpya, utaalam mpya .
Mfano wa technologia mpya ni kampuni za simu, mfano huu naupenda kwakua ni moja ya mifano bora kabisa ya faida za FDI.
Nchi hufanya nini kuvutia wawekezaji, na hii sio Tz tu, bali dunia nzima.
1 Mambo kama kutengeneza EPZ jambo unaona Tz imejikita sana, mfano bagamoyo na maeneo mengine zinapo jengwa.
2: misamaha ya kodi
3: kodi zisizokua juu
4: kutengeneza kanda maalum za uchumi.
5: utoaji wa ardhi
6: ruzuku za ardhi
7: ruzuku za mikopo
Nakadhalika
ukiangalia kwa jicho la kishabiki unaweza kusema nchi inauzwa, lakini kuvutia wawekezaji kuna fanyika dunia nzima.
Dunia ya sasa ndio ilivyo hakuna atakaye fanya tofauti, labda kuongezea pale kupunguza huku.
Hatua zinazochukuliwa na matendo yanakubalika kwenye macho yangu, pia nataka juhudi hizi ziendelee, na siamini kama kuna mwingine anayeweza kuendeleza mipango hii endelevu.
Napongeza Tz kupata FDI nyingi kuliko nchi yoyote, kina Dangote na wenziwe wa aina yake tunawakaribisha sana Tz waje kujenga viwanda, na biashara nyingine zitakazo ongeza ajira.
Japo kuna mapungufu kwenye baadhi ya mambo kama ufisadi, ambapo tunategemea CAG mpya atayatumia mamlaka yake kwa ukamilifu zaidi ya aliyepita. Jitahada endelevu za serikali katika kutengeneza mazingira ya uchumi kukua tunayapongeza.
Kutokufahamu kwako mambo kunaweza kukufanya usielewe nini kinaendelea, na hivyo kupunguza uwezo wako wa kuziona fursa, na kuzifanyia kazi.
Tujitahidi kufahamu mambo, ama kupunguza ujinga.
Sifa zote na shukrani ni za Mola.
http://en.wikipedia.org/wiki/Foreign_direct_investment
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments