TUME ya Taifa ya Uchaguzi-NEC, imetoa ufafanuzi zaidi kuhusu ushiriki wa Wanajeshi katika uboreshaji wa zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Kupiga Kura, linalotarajiwa kuanza kwa majaribio Jumatatu ijayo, katika Majimbo Matatu nchini.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Tume, kutakuwepo na Wanajeshi Sita wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania, JWTZ, ambao kazi yao itakuwa ni kusaidia shughuli za Lojistiki kama vile kuhamisha Vifaa kutoka Kata Moja kwenda nyingine.
Pia Wanajeshi hao watasaidia katika shughuli za kufanya matengenezo Madogo Madogo ya Vifaa yanayoweza kujitokeza wakati wa zoezi la uandikishaji.
Taarifa inasisitiza kuwa Wanajeshi hao hawatakuwepo kwenye vituo vya Uboreshaji wala hawatahusika na zoezi la uandikishaji kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoiti hivi karibuni.
Aidha, katika mkutano na Vyama vya Siasa uliofanyika juzi jijini Dar es Salaam ulifafanua kuwa watendaji watakaohusika katika zoezi hilo ni maafisa Waandikishaji na wasaidizi wao, Waandishi Wasaidizi, Wataalamu wa fani ya TEHAMA na wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments