Abdallah Kibaden aliwahi kuwa kocha wa Simba, Kagera Sugar na Ashanti.
Kocha wa zamani wa klabu ya Simba Abdalla 'King' Kibaden amefariki dunia leo.
Kibaden ambaye alichaguliwa kuwa kocha wa Simba mwaka 2013, pia aliwahi kuwa kocha wa Kagera Sugar na Ashanti United.
Baada ya Sunderland kufungwa 5-0 na Yanga 1968 iliamua kubadilisha kikosi chake kwa kuwaondoa wachezaji wakongwe na kusajili wachezaji chipukizi.
Miongoni mwa chipukizi hao walikuwa Abdallah Kibaden, Willy Mwaijibe, Omary Gumbo,nk. mwaka huo Abdallah Kibaden alichaguliwa katika timu ya taifa ya Tanzania na vile vile alikuwa mwanasoka bora wa Tanzania.
Mchezaji huyo ambaye ana elimu ya ufundi magari Daraja la Pili (Motor Vehicle Mechanics Grade II) amewahi kuajiriwa katika kampuni mbalimbali, ajira ambazo kupatikana kwake kulichangiwa na kipaji chake cha soka.
Wasifu wa Kibaden
Oktoba 11, 1949: Alizaliwa Kiburugwa, Mbagala jijini Dar es Salaam.
1959: Alitungiwa jina 'Kibaden' na watoto wenzake kwa kucheza soka ya nguvu akiwa mdogo na mfupi. Jina lake halisi ni Abdallah Athuman Seif. Kibaden maana yake ni kitu cha baadae.
1969: Alijiunga na Simba FC, iliyokuwa ikiitwa Sunderland.
2011: Alikwenda Hijja.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Taarifa zaidi kuhusu kifo chake zinakuja…
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments