[wanabidii] Niwakumbushe Ya Miaka Ya 90: Kisa Cha Chifu Fundikira Na NCCR...

Thursday, December 11, 2014


Ndugu zangu,

Kwenye maktaba yangu kuna kumbukumbu ya habari ya kwenye Daily News August 21, 1991. Ni miaka ya mwanzoni mwa vuguvugu la mageuzi nchini. 
Mimi ndio nilikuwa sijatokwa hata na vumbi la JKT, nilimaliza Juni, 1991, Operesheni Kambarage.

Nakumbuka kukisoma kisa cha Chifu Abdalah Fundikira aliyeondolewa uwenyekiti wa NCCR na wenzake akina Prince Bagenda na Mabere Marando wakati Chifu akiwa ziarani. Kisa?

Akina Bagenda na wenzake wa National Committee of Constitutional Reform ( NCCR) , ni kama UKAWA vile ya wakati huo, waliamua kumuengua Chifu kwenye kiti chake kwa vile Chifu alikusudia kupangisha nyumba yake kwa NCCR kwa gharama ya shilingi elfu hamsini kwa mwezi! Mabere Marando akajitolea nyumba yake iwe ofisi, bure!

Kesho yake, Daily News likaripoti, kuwa Chifu Fundikira ametua Dar akitokea ziara ya Uingereza na Marekani na kuwashangaa akina Prince Bagenda na wenzake. Chifu akawaambia wanahabari, kuwa hao akina Bagenda na Marando hawana mamlaka ya kisheria ya kumwondoa kwenye kiti chake. Alisema, Kamati yenyewe kwa maana ya NCCR haiko rasmi kisheria, na uwanachama ni wa hiyari na usio rasmi. Na Chifu akaongeza kusema, kuwa kimsingi NCCR yenyewe si halali kisheria kwa vile haijasajiliwa. Kabla ya hapo Mabere Marando alimshutumu Chifu kwa kulitumia jukwaa la NCCR kupanga mikakati ya kuanzisha chama chake.
( Daily News 21 na 22 Agosti, 1991(

Maggid,
Iringa.

http://mjengwablog.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments