[wanabidii] MAZIWA HALISI YA AZAM.....

Thursday, December 04, 2014

MAZIWA HALISI YA AZAM.....

Nilitumia maziwa haya wiki moja iliyopita wakati wa mchana maeneo ya Kariakoo... Nusu saa baadaye niliomba hifadhi Msikitini ili kupata access ya maliwato kwani nilikuwa naendesha kwa fujo sana huku tumbo likiunguruma kama katalina.

Siku ya jana nilibahatika kuagizwa na mama chanja wangu nimletee box la maziwa, nilimtajia orodha ya maziwa akasisitiza nimletee maziwa ya mzalendo mwenzetu Azam. Yeye alipomaliza kunywa glasi ya kwanza alikimbia maliwato kutapika. Ananiambia alipomaliza kunywa alipatwa na kichefu chefu kisicho cha kawaida....

Hapa napenda kufahamu kama kunakuwa na ukaguzi wa bidhaa zilizoko sokoni hasa baada ya mzalishaji ama msambazaji kupewa cheti cha Ubora (TBS) na kile cha TFDA....

Inawezekana wahanga wapo wengi ila hawajajitokeza kusema...

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments