TAREHE 22 / 12 / 2014 majira ya jioni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amelihutubia taifa kupitia wazee. Amezungumzia mambo mengi ila nitapitia moja tu la kashfa ya Escrow. Habari ya Escrow ni ndefu na ina mambo mengi mchanganyiko na ya kiufundi sana. Pamoja na kuwa mambo mengi ni ya kiufundi bado ukitulia vizuri na kulipitia kwa umakini sakata hili unaweza kutoka na mambo machache lakini yenye kueleweka zaidi kiasi ambacho unaweza kumuelewesha hata mtu wa kawaida akakuelewa. Kutokana na hilonataka nieleze kwa ufupi wenye kueleweka dondoo chache kutoka hotuba ya rais kuhusu Tegeta ESCROW akaunti.
( 1 ) KULIKUWA NA PESA UMMA.
Sijui kwanini Rais amerudia kusema kuwa pesa hazikuwa za umma. Katika mambo ambayo hayana utata katika jambo hili ni hili swali la pesa kuwa za umma au lah. Ni kitu chepesi sanakupata majibu ya swali hili lakini sijui kwanini viongozi hasa rais na Waziri Mkuu hawataki kulielewa. Sijui ni kwa makusudi au kwa kulinda heshima kwakuwa serikali ilishakuwa na msimamo huo tangu mwanzokabla hata ya skendo yenyewe. Nafikiri ni kulinda heshima. Rais amesema pesa ile haikuwa ya umma halafu baadae akasema kulikuwa na kodi ya serikali ambayo haikulipwa na akasema tayari mamlaka ya mapato wameanza kufuatilia kodi zile na kuwa IPTL wameshakubali kulipa. Nini maana ya kauli hii na ni maana ya kauli kuwa hakukuwa na pesa ya umma.Kama hakukuwa na pesa ya umma TRA wanadai hela ya nini na kwa ajili ya nani.Kama rais angesema kulikuwa na pesa ya mwekezaji pamoja na ya umma kingeeleweka zaidi. Haiwezekani ukasema hakukuwa na pesa ya umma halafu ukasema kulikuwa na kodi ya serikali ambayo haikulipwa. Hiloni moja.
( 2 ) MAHAKAMA KUU HAIKURUHUSU PESA ITOLEWA KWA IPTL.
Rais amesema mahakama iliruhusu pesa itolewa kwa IPTL. Mahakama haikusema hivyo. Kwanza ieleweke kuwa mgogoro uliokuwa mahakama kuu yaTanzaniambele ya jaji Utamwa si kati IPTL na Tenesco. Mgogoro uliokuwa kwa Jaji Utamwa ni kati ya Mechmar na VIP Engineering. Hili hata rais mwenyewe amekiri kuwa Rugemalira ambaye ndiye VIP Engineering ndiye aliyepeleka mgogoro huo mahakamani kulalalmikia mwekezaji mwenzake Mechmar. Wakati mgogoro huo ukiwa mahakamani VIP Engeneering ambaye ndiye alikuwa mlalamikaji aliamua aachane na mgogoro na auze hisa zake kwa mechmar ambaye ndiye aliyekuwa akilalamikiwa. Mahakama kuu baada ya kuona wenye kesi wamekubaliana ikasema kuwa kama wamekubaliana kesi imeisha na mambo yote kuhusu IPTL yakabidhiwe kwa Mechmar.Ikumbukwe IPTL inaundwa na watu wawili Mechmar na VIP Engineering ambao ndio walikuwa na kesi. Hivyo mahakama kusema hivyo ilimaanisha kuwa malizilizokuwa zikimilikwa na VIP Engineering zikabidhiwe kwa Mechmar ili abaki mmiliki wa IPTL peke yake. Kwa hiyo Mechmar akabaki ndiye mmiliki pekee wa IPTL. Kumbuka kuwa Tanesco hakuwa anahusika kwa namna yoyote katika mgogoro huo kwa kuwa haumhusu. Maana ya hili ni kuwa mgogoro wa wa IPTL na Tanesco haukuwa umeguswa kwa` namna yoyote na hukumu hii ya mahakama ambayo ilikubnali wenye kesi kumaliza tofauti zao. Kama haukuguswa kwa`namna yoyote ile basi hata ESCROW Akaunti ambayo inatokana na mgogoro kati ya Tanesco na IPTL na si Mechmar na VIP Engeneering waliomaliza kesi pia haikuguswa na hukumu hiyo. ESCROW akaunti ilikuwa kwa ajili ya mgogoro wa IPTL na Tanesco na si mgogoro wa Mechmar na VIP Engineering. Hukumu ambayo ingetoa zile pesa ni hukumu kati ya Tanesco na IPTL na si hukumu kati ya Mechmar na VIP. Mgogoro wa tozo ambao ni wa Tanesco na IPTL ndio mgogoro uliozaa ESCROW Akaunti, mgogoro wa VIP na Mechmar haukazaa Escrow Akaunti na wala ECSROW haiuhusu. Iweje sasa hukumu ya mgogoro ambao hauhusiani na ESCROW ndio iruhusu pesa kutoka BOT. Ni wazi mahakama haikusema hivo isipokuwa iliposema mali na shughuli zote zikabidhiwe kwa IPTL ilikuwa ikimaanisha shughuli zote ikiwamo na mgogoro wa ESCROW ukabidhiwe kwa IPTL ili iendelee nao. Ina maana ilikabidhiwa na mgogoro ambao kuumaliza kwake ili pesa itoke ni baada ya makubaliano na Tanesco na si baada ya hukumu.Hakuna popote katika hukumu ile paliposemwa hela apewe IPTL isipokuwa ilisemwa Mechmar alikabidhiwe shughuli za IPTL mgogoro ikiwa shughuli mojawapo na si pesa.Si sawa kusema mahakama ilisema pesa apewe IPTL
( 3 ) TANESCO ILISHINDA KESI MAHAKAMA YA KIMATAIFA.
Tanesco ilifungua shauri la kulalamikia tozo mahakama ya biashara ya`kimataifa na ikashinda japo si kwa kiwango ilichokuwa inataka. Kwa maana hii ni kuwa kamaTanesco ilishinda lakini ikakosa pa kulalamika zaidi kwakuwa mahakama hiyo haina rufaa wala kuomba marejeo(review) basi hukumu ile ndo ilitakiwa kufuatwa na si vinginevyo. Na kwa kufuata hukumu ile Tanesco ingeokoa kiasi cha pesa kwakuwa hukumu hiyo ilipunguza tozo ambayo tanesco walipaswa kulipa kwa IPTL. Kwa kufuata hukumu hiyo Tanesco ingeokoa fedha kuliko hivi ambavyo fedha zote zimechukuliwa na IPTL. Ajabu ni kuwa hukumu hiyo haizungumzwi na kwanini haikufuatwa pia wahusika wamekaa kimya kama haikuwahi kuwapo.
( 4 ) RAIS HAKUWA MKALI KWA WAKWEPA KODI.
Rais amesema kwenye pesa iliyotolewa ESCROW kulikuwa na pesa ya kodi ambayo haikulipwa lakini akasema hatua walizochukua mpaka sasa ni kuwa TRA wanaendelea kudai kodi hizo. Rais hajasema lolote kuhusu kwanini kodi haikulipwa tangu awali. Ameanza kushughulika na hatua ya pili kabla ya hatua ya kwanza.Hatua ya kwanza ni swali la kwanini walikwepa kodi huku wakijua kuwa kufanya hivyo ni kosa.Tulitarajia kusikia hatua za kijinai. Hatua ya pili ndo ije hiyo sasa ya TRA kuanza mchakato wa kudai hizo kodi. Huwezi kumdai kodi aliyekwepa kodi kabla hujamchukulia hatua za kutolipa kodi. Ni sawa na mwizi kuiba radio ukaagiza jeshi la polisi waifuate ile radio kwake halafu iishie hapo.
MWANDISHI WA MAKALA HAYA, Bashir Yakub, NI MWANASHERIA
0784482959 / 0714047241
-- ( 1 ) KULIKUWA NA PESA UMMA.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments