[wanabidii] Fwd: OPRESHENi-FUTA?

Sunday, December 21, 2014
>
> OPRESHENi-FUTA?
>
> (Dr.Muhammed Seif Khatib)
> Nimeangalia maana ya neno 'opresheni' na 'futa' katika kamusi.Kwa nini?
> Kwa sababu chama kimoja cha siasa kilikurupuka na kuyatimia maneno hayo.
> Wao ni weledi wa kufua maneno kama hayo.Mnakumbuk 'opresheni sangara?'
> Ilipoanzishwa sangara wakaliwa na furu.Opresheni ni shughuli ya dharura
> zinazofanywa kutatua tatizo la jamii kwa muda.Walakini upo wapi? Taaib!
> Kuna dharura.Hipo dharura ya kuiondoa CCM mafarakani?Tatizo gani lipo?
> La CCM kuweka amani na utulivu nchini?La kuwawekea watu miundombinu? Lipo neno 'futa' lakini chama cha wapinzani kilichojaa wasomi kimetumia neno la Kimombo la 'delete' lenye maana 'kuondoa kitu kilichohifadhiwa katika kompyuta'Bila ya shaka wao waikusudia kuiondoa CCM katika madaraka.Lakini neno futa kutoka katika kamusi ya Kiswahili lina maana zaidi ya nane.Futa kwa kitu kilichoandikwa.Futa ni kuchomoa kitu katika ala.Futa ni
> kutoa maji yaliyoingia katika chombo cha majini.Futa ni kuanguka kwa kitu kama nyumba au mnanzi.Futa ni kususia kitu.Futa ni aina ya nyoka mkubwa
> mwenye mdomo mweusi.Futa ni pande la shahamu. Futa ya nane ni chuki au uhasama.Tumeona utajiri la ya Kiswahili wakati kambi ya upinzani wameona
> watumiye lugha ya Kimombo wakati wanaongea na Waswahili.
> Hata hivyo nia yao ni kufanya shughuli ya dharura kuifuta au kuiondosha CCM madarakani. Kama hilo haitoshi la kuiendesha opresheni hiyo wakaunda
> UKAWA ili washirikiane waiangushe CCM. Uchaguzi wa serekali za Mitaa
> Vitongoji na vijiji ulikuwa mtihani wa kwanza wa kuona matokeo ya Opresheni-futa CCM.Uchaguzi huu ulipima nguvu za UKAWA dhidi ya CCM. Sehemu kubwa ya uchaguzi umefanyika. Sehemu zilizobaki zaweza kumalizika leo. Hata
> hivyo muelekeo unaonesha CCM inapeta. Hakuna UKAWA hakuna Opresheni
> Delete. Wote wamegaragazwa. Hivi yanajulikana kama katika ngome za Upinzani bado CCM imeongezeka?Yepi matokeo ya Arusha,Moshi,Mbeya na baadhi ya majimbo ya Wapinzani? Kote huko CCM inongoza.Hata katika
> maeneo mengi ambayo wapinzani wamedondoa ni makosa ya wanachama wa CCM wenyewe.Wengine wamenuna.Wengine wamenunuliewa.Wengine wamezembea na wengine ni mamluki.Hayo tuwaachiye viongozi wa naeneo
> wayashughulikiye. Sasa ni miaka ishirini na tano tangu upinzani uanze na
> vyama vinavyojiita vikubwa na vyenye misuli navyo havifudafu mbele ya CCM.
> Bado vyama vya upinzani kila kukicha vinazliwa.Kwa nini? Kwa sababu watu hawaridhiki na kasi na uwezo wa vyama upinzni hivyo kila kukicha vinaundwa?
> Lakini ujio wa vyama upinzani pamoja na opresheni zao za sangara au delete
> na nyingi zijazo hawaziwazimi usingizi CCM.Chama kikija peke yake
> kitaangushwa au vikija kwa ubiya kama UKAWA vitagaragazwa.Kwa nini?
> Chama cha MAPINDUZI hakifanyi kazi kwa kukurupuka.Hakina kitu
> Opresheni.Chama hiki kimejipanga vizuri na kutoandika mtandao wake
> nchi nzima. Kinakwenda kwa watu mwaka mzima na hakisubiri uchaguzi
> hadi uchaguzi.Watu wengi wenye shida na taabu Wapo vijijijni siyo mijini.Chama hiki kwa kujuwa hilo serekali yake na chama chenyewe kinaweka uzito mkubwa
> wa kuwaondolea watu wake shida,tabu na kero.Huku ndiko kwenye shida za watu za maji,umeme,tiba,miundo mbinu pembejeo na kadhalika.Wapinzani w
> wanawaomba kura wananchi wa vijijini bila kuwahudumia.Sawa na kutaka
> wakame maziwa kwa ng'ombe wasiopewa majani?Hili haliwezekani.Wapinzani
> hawatafiti sababu ya wao kuangukia pua!CCM inaongoza hadi sasa katika
> uchaguzi wa serekali za mitaa,vijiji,na vitongoji. Matokeo yote bado hayajatoka.Lakini itakuwa miijiza kama baada ya uchaguzi wote kwisha vyama
> UKAWA vyote kwa pamoja au mmoja vije viishinde CCM.Haliwezekani.Ile 'opreshni-delete' CCM iliyotumia ndege ya helkopta ni matumizi mabaya ya
> fedha za kodi.matajiri wao,fedha za 'mabwana' zao huko nje.CCM ni mbuyu
> haitikisiki na haiyumbi. Wakati tunasubiri matokeo ya mwisho uchaguzi hadi sass CCM inakadiriwa kuongoza kwa asilimia 81.96 katika vijiji,Asilimia
> 83.3 katika vitongoji na Asilimia 68.9 katika mitaa.Kwa matokeo haya ya
> awali kile chama kililichotangaza na kutekeleza 'OPRESHENI-DELETE'
> inadhani imefanikiwa?Chama unachokifuta kinakubaliwa na asilimia kubwa
> ya wananchi?
>
> O
>
>
> Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments