SAHAU
(Dkt.Muhammed Seif Khatib)
> Sahau ni kipotelewa na kumbukumbu .Jambo hili lina uzuri wake na ubaya wake.Uzuri > kwa wale wanaofikiwa na majanga na misiba ya kufiwa na wapendwa wao, sahau huwapa > afuweni ya kutokana na majonzi, simanzi inayosononeshwa na maumivu makali ya moyo. > Bila sahau leo watu wangelia na kubwata kwa kwikwi na kite usiku na mchana.Milizamu ya machozi ingetosa macho na skurubu zinazoshikilia bawaba za chemchem na visima > zingeachana kwa wingi wa machozi na uchovu. Machozi yangekauka.Sauti zingepotea, nguvu za mwili zingemalizika.Wajihi na sura za wapendwa wetu zingetuzuru katika > maskani yetu,majumbani mwetu na nyoyo zetu.Sidhani kama tungeweza kuwa na nguvu > za kula, kuongea, kufanya kazi au hata kufanya ibada. Nyumba zetu zingegubikwa na > misiba ya dhuria wetu.Mtoto angemlilia mama au baba.Baba au mama angemlilia bibi > au babu. Jamii ingesita kufanya maendeleo kwa sababu ya misiba na simanzi.Hivi nani > angethubutu kuposa au kuposwa katika nyumba yenye matanga.Kwaajili hiyo koo na familia zisingendelea na maisha yangekuwa mafupi na dunia isingekuwa na shamrashamra > ya starehe na anasa.Misiba ingeunganishwa.Sala na ibada za kuwaombea wafu ingekuwa > kila siku.Sahau imesaidia kuwasahau marehemu waume zetu, wake zetu, watoto wetu na > waitifaki na wapendwa wetu.Tumewasahau wasanii na wanamichezo nyota.Tumewasahau > Marais na Masultani ambao watuitapo huona fahari.Wapo watu ambao kusahu kwao > siyo kosa wala tatizo.Hawa husamehewa na jamii.Watu wazima wengine hupatwa na > ugonjwa wa kusahau.Husahau sura za watu wa karibu yao au katika maongezi hapana > alikumbukalo.Watoto kwa uchanga wa bongo na fikra nao husahau kila kitu.Sahau haifai > kwa mambo mengine.Huwezi kidaiwa fedha au mali ya watu ukaacha kulipa kwa kudai > kuwa umesahau!Ama unakacha kutii sheria na kudai umesahau!Sahau haipaswi kutumiwa > kama kisingizio ya kutenda uhalifu ama utovu wa adabu. > Neno ukoloni ni mtindo wa nchi moja kuitawala nchi nyingine.Ukolono hauna kabila, > rangi,jinsia wala dini.Kinyume chake ni Uhuru ni hali ya kuishi bila kutawaliwa na mtu > mwingine au nchi nyongine.Yawezekana Watanzania tukiacha watoto na wale > wazee wenye maradhi ya kusahau maneno hayo mawili wameyasahu maana yake > na uhusiano wake na nchi ya Tanganyika.Wale wanaojidai wamesahau itakuwa > hawakutenda haki.Wapo watu waliojitolea katika uhai wao kuanzisha vuguvugu la kudai > Uhuru kutoka kwa wakoloni.Na kila jambo lina kiongozi wake wa kiliongoza.Uhuru wa > Tanganyika uliongozwa na uweledi Nyerere. Lakini chombo cha kukitumia ni chama cha > siasa cha TANU.Hivi Nyerere na TANU ndiyo iliyokuwa alama ya matumaini ya > Waafrika.Kwa upande mmoja kulikuwa na uongozi shupavu uliojizatiti na umma mkubwa > ulioandaliwa kifkra kuwa Tanganyika wenyewe ni Waafrika na lazima wajitawale.Ukoloni > wa Kingereza lazima ufunge virago.TANU ilipigania Uhuru kwa miaka saba.Lakini nani > walioshiriki? Wengi ya wapiga kura walikuwa wakulima,wavuvi,wafugaji,wafanyakazi, > wafanyabiashara na wachuuzi.Ni wao waliojitolea kwa hali umali kukiimarisha chama > cha TANU.Sauti zao za wanyonge wakazipaisha.Kila uchaguzi Waafrika wakajaza > visanduku pomoni kwa wagombea wa TANU.Kwa uongozi bora ukoloni tukautimua.Tanganyika ile iliyotawaliwa na wageni tokea Warenu,Wadachi,Waarabu > na mwishoni Waingereza tokea ardhi na nchi ya Tanganyika iwepo ni tofauti na ile > iliyokmbolewa na TANU.TANU na ASP chama ukombozi wa Tanganyika na Zanzibar > ikaikabidhin Tanganyika na Zanzibar kwa warihi halali wa CHAMA CHA MAPINDUZI.Keshokutwa miaka hamsini na tatu Uhuru wa Tanganyika unatimia.Maisha ya watu ukilinganisha na wakati wa ukoloni ni sawa?Hatusemi kuwa maisha ya sasa ni pepo lakini pia siyo jahanamu.Hivi tarehe 8 Disemba mwaka 1961 Tanganyika ilikuwa na shule ngapi za praimari na sekandari?Kulikuwa na Vyuo Vikuu na asasi ngapi?Waafrika > wenye shahada ya kwanza,ya uzamili na uzamivu wangapi? Maprofessa Waafrika > ni wangapi?Idadi ya wanafunzi tokea chekechea hadi vyuo vikuu ni wangapi?Silku moja kabla Uhuru Tanganyika ilikuwa na vituo vya afya,zahanti,hospital za wilaya,mikoa > za rufaa zilikuwa ngapi na sasa baada ya utawala TANU na CCM mrithi halali zipo ngapi?Miundo mbinu za barabara zenye lami zilikuwa kilomita ngapi na baada ya miaka hamsini > na tatu urefu imepanuka kiasi gani.Labda kwa lugha nyepesi kutoka Dar es Salaam > kwenda Mpanda kwa utachukua siku ngapi? Au kutoka Manda kwenda Dar huchukua > siku ngapi?Ama tuseme unaweza kutumia leo gari ndogo kutoka Namtumbo hadi Dar > kupitia Dodoma.? Kama ndio tarehe 8 Disemba mwaka 1961 ingewezekana kuja > Dar kwa gari kutoka ileje kupitia Mtera hadi ?Dar es Salaam ya siku ya Uhuru ndiyo > ilivyo leo? Barabara zake, majengo yake,mandhari yake na utanashati watu wake!Unapata wasaa wa kuangalia magari ya Dar es Salaam ya milikiwa na nani? Nadhani si Magiriki, si Wazungu,si Wahindi,si Waarabu ni Wamatumbi.Waone asubuhi > wanaume watanashati wamenyonga mijusi yao shingo ni na pamba imekubali > wanasokota sukani,viyoo vimefungwa na viyoyozi vinapuliza.Waangaliye akina > mama vijana,makamo na wazee na utanashati wao mkono wa kulia kashika sukani > mkono wa shoto kikombe cha maziwa anapiga funda polepole.Ni hawa hawa jioni wakirudi > waangaliye jinsi wanavyoingia katika mahekalu yao fahari.Ipo gari ya mume, ya mke na y > mtoto mwanamke na mwanamume, zote zinafunguliwa geti na kuingizwa. Miaka saba > ya kudai Uhuru ni michache kuliko miaka hamsini na tatu kufakamia matunda ya Uhuru! > USISAHAU kuwa mafanikio yote hayo ni kazi ya TANU na ASP na kurithishwa na > CCM.
--Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CACMr6QjkSKOd427AiR5TJLn88zYrmAYJeX_pM2Uf30bAnrAuRA%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments