[Mabadiliko] Mkurugenzi Sengerema Atimuliwa Kazi kwa kuharibu Uchaguzi Buchosa.

Wednesday, December 17, 2014

Baada ya kuahirisha uchaguzi wa serikali za mitaa siku ya jpili iliyopita na kutangaza utafanyika siku ya jmosi kabla ya kubadilisha tena ghafla na kulazimisha uchaguzi ufanyike jana, aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema amefukuzwa kazi leo.

Moja ya sababu zilizopelekea kutimuliwa kwa mkurugenzi huyo ni kukubali kuyumbishwa na wanasiasa wa chama tawala, hasa mbunge wa Buchosa aliyeshinikiza uchaguzi uahirishwe ili ccm ipate nafasi ya kujiweka vizuri baada ya kuonekana kuelemewa vibaya na chadema.

Dalili za mbunge wa Buchosa kushiriki kuhujumu uchaguzi kupitia mkurugenzi aliyefukuzwa zimekuja kudhihirika baada ya mbunge huyo kuoneka ghafla sehemu mbali mbali jimboni jana akigawa pesa kwa viongozi wa chama chake ili zisambazwe kwenye vitongoji kwa ajili ya kuwapa wapiga kura ili kupunguza makali ya kuadhibiwa na chadema.

Uchaguzi huo umeisha jana na chadema wamepata viti karibia nusu ya vijiji  81 vilivyopo toka 8 vya 2009, na vitongoji zaidi ya 105 kati ya 237 vilivyogombewa.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CADVpsxQPXq0HUgy6LmhTE27q-oP6oXWOtNvaUbDxQs6WvZdRVw%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments