[Mabadiliko] Mama Salma: Rais Kikwete ana hasira, wanaosema mpole hawamjui

Wednesday, December 03, 2014

Tujikumbushe

JF

NA BASHIR NKOROMO, LINDI


MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCN, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametoboa siri kwamba mumewe, Rais Jakaya Kikwete pamoja sura yake kujawa haiba ya ucheshi wa mara kwa mara lakini kwa tabia ana hasira. Amesema, Rais Kikwete hukasirika sana anapoona au kusikia mtu au mtendaji katika Chama au serikali anafanya mambo ya hovyo au ya kizembe hasa katika masuala ya kazi.


Mama Salma Kikwete ametoboa siri hiyo, leo Februari 18, 2013, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kikwetu Kata ya Mbanja akiwa katika ziara ya kukagua, kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama na kuwashukuru wana-CCM wa Lindi mjini kwa kumchagua kuwa mjumbe wao wa NEC.

"Siyo kweli kwamba Rais Jakaya Kikwete siyo mkali, japokuwa ana sura yenye haiba ya ucheshi wa mara kwa mara kwa kila mtu, lakini ni ana hasira, tena sana pale mtendaji au mtu yeyote anapombaini kwamba anafanya mambo ya hovyo au ya kizembe katika kazi za Chama au serikali yake", alisema Mama Salma Kikwete.


Mama Kikwete akitoa ufafanuzi, baada ya mshereheshaji mmoja kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Lindi mjini Muhsin Ismail, kusema kwamba Rais Jakaya Kikwete ni mpole wa kupindukia na kuuliza umati wa wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo kwamba je ni nani amewahi kumuona amenuna.


"Natoa ofa kama hapa kuna mtu aliyewahi kumuona mpendwa wetu, Rais Kikwete amenuna anyooshe mkono. Akitokea ntampa sh. elfu moja hapa hapa... Kwa mara ya kwanza, ya pili unaona hakuna", alisema Muhsini.

Wakati akiendelea kusema hivyo, mtu mmoja kwenye mkutano huo alinyoosha mkono, lakini Muhsin akakataa kumpa zawadi yake kama alivyokuwa ameahidi. "Aaa wewe sikupi zawadi", alisema Muhsini lakini papo hapo akakatishwa na Mama Mama Kikwete. "Hata kama humpi hiyo zawadi, sawa. lakini Siyo kweli kwamba Rais Jakaya Kikwete hakasiriki na siyo mkali. Japokuwa ana sura yenye haiba ya ucheshi wa mara kwa mara kwa kila mtu, lakini ana hasira, tena sana pale mtendaji au mtu yeyote anapombaini kwamba anafanya mambo ya hovyo ay ya kizembe..." alisema Mama Kikwete

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CACChgVReg0PfSuec3gmiHZqy%2B3iU7J4CMHNa02LKej23%3DLHo8g%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments