[wanabidii] Watanzania Kunyanyasika Nchi za Nje Mbunge mmoja leo amehoji kwanini watanzania wananyanyasika nchi za nje haswa Msumbiji na Afrika Kusini ambao tuliwasaidia katika harakati zao za Ukombozi ? Pia kahoji kwa nini ada ya kukukaa kwenye nchi nyingi hata zile mara fiki ni kubwa kuliko wao wakija nchini kwetu ? Waziri kamwambia Suala la ada linapangwa na wizara ya nchi husika watajadiliana kuona inakuwaje . Suala la Watanzania kusumbuliwa haswa Nchumbiji na Afrika Kusini ni kweli lakini akasema watanzania wengi wanaosumbuliwa hawaendi huko kwa njia halali na hata wanapokua kuhalali hawalipi kodi au kufanya shuguli halali kisheria hii ndio tatizo moja kubwa . Mie naongezea , watanzania tukienda nchi za watu tutafute taarifa za kutosha kutokea nchini kwanza kupitia balozi na wizara ya mambo ya nje , kule unaweza kukuta vyama vya watanzania au afrika mashariki na vitu vingine mbalimbali ukifika watakupokea vizuri na kukuelewesha mambo mengi hapo utakaa kwa amani . Wenzetu wakija kwetu wanaha

Friday, November 14, 2014
Watanzania Kunyanyasika Nchi za Nje 

Mbunge mmoja leo amehoji kwanini watanzania wananyanyasika nchi za nje haswa Msumbiji na Afrika Kusini ambao tuliwasaidia katika harakati zao za Ukombozi ?

Pia kahoji kwa nini ada ya kukukaa kwenye nchi nyingi hata zile mara fiki ni kubwa kuliko wao wakija nchini kwetu ?

Waziri kamwambia Suala la ada linapangwa na wizara ya nchi husika watajadiliana kuona inakuwaje .

Suala la Watanzania kusumbuliwa haswa Nchumbiji na Afrika Kusini ni kweli lakini akasema watanzania wengi wanaosumbuliwa hawaendi huko kwa njia halali na hata wanapokua kuhalali hawalipi kodi au kufanya shuguli halali kisheria hii ndio tatizo moja kubwa .

Mie naongezea , watanzania tukienda nchi za watu tutafute taarifa za kutosha kutokea nchini kwanza kupitia balozi na wizara ya mambo ya nje , kule unaweza kukuta vyama vya watanzania au afrika mashariki na vitu vingine mbalimbali ukifika watakupokea vizuri na kukuelewesha mambo mengi hapo utakaa kwa amani .

Wenzetu wakija kwetu wanahakikisha wanapata taarifa zote muhimu hata maeneo ya kutembelea na kinga mbalimbali kwa ajili ya afya zao na mawasiliano na balozi au wawakilishi wan chi zao ,

 Je sisi tunafanya hivyo tukienda kwao ? Tubadilike .


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments