[wanabidii] USHAURI. NI TUKIO LA KWELI, LINAHITAJI MAAMUZI SAHIHI

Sunday, November 16, 2014

ANAOMBA USHAURI. NI TUKIO LA KWELI, LINAHITAJI MAAMUZI SAHIHI.

Dada jirani yangu, amechumbiwa. Wametambulishana na kukamilisha taratibu zote. Mipango ya harusi ikawekwa vizuri. Ndoa imepangwa kufanyika Desemba 20, 2014. Vikao vya harusi vimeanza tangu Septemba 2014.

Wachumba hawa walikubaliana wasikutane kimwili hadi siku ya ndoa yao. Juzi ijumaa walienda kuangalia afya zao, mwanaume akakutwa ameathirika na Ukimwi. Huyu dada tangu juzi halali, kilio tu. Wazazi wake walifariki zaidi ya miaka minne iliyopita. Anaona ni aibu na balaa.

Nikiwa kama mjumbe wa kamati ya harusi, mpaka sasa tunawaza cha kufanya. Kikao tumepanga kufanya jumatano ijayo. Sasa sijui tusemeje kwenye kikao na Kanisani. Michango ya watu tunayo.

Naomba ushauri jinsi ya kuli-handle suala hili. Tafadhali, jitahidi kutupa mawazo kwani huyu dada anawaza kupotea nyumbani asionekane tena, sijui anataka kupotea kwa kujiua au kutoroka tu, sijui. Ushauri tafadhali.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments