[wanabidii] TAMKO LA JUVICUF KUHUSU UTAFITI ULIOFANYWA NA TWAWEZA KUHUSU HALI YA KISIASA NCHINI

Thursday, November 13, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAMKO LA JUVICUF KUHUSU UTAFITI ULIOFANYWA NA TWAWEZA KUHUSU HALI YA KISIASA NCHINI.

JUVICUF inapenda kuchukua fursa hii adhimu kuwashukuru kwa kufanya utafiti unaohusu hali ya Kisiasa nchini. Pamoja na shukrani hizo, JUVICUF haikubaliani sana na kilichosemwa na TWAWEZA katika majibu yao mbali mbali ya Maswali yao ya Kitafiti.
SABABU ZA KUUPINGA UTAFITI.
1. Utafiti umefanywa kwa njia ambayo washiriki (Respondents) hawako wazi sana . Mfano wametumia njia ya Simu kuwauliza , jambo ambalo linadhihirisha kuwa washiriki wanaukaribu na watafiti jambo ambalo kitafiti linaweza kuwa si zuri sana (Bias) Unahoji mtu ambae unajua itikadi yake na mtazamo wake wa kisiasa.Maana umepata wapi namba yake ya simu?. Kama wanajitetea kuwa waliohojiwa hawana ukaribu na watafiti. Tulitarajia kuona waki acknowledge TCRA kwa kuwapatia namba za simu za Washiriki. (Utafiti ni Critically biased).

2. Utafiti umebase katika idadi ya washiriki (Quantity) pasi na kuangalia na uhalisia wa maeneo husika (Selection of sample). Nchi yetu imegawanyika kikanda na kimikoa juu ya wananchi wanavyounga mkono wanasiasa na vyama vya siasa (Strong holds za Vyama vya Siasa) . Ikiwa utafiti unabase katika idadi ya washiriki, lakini swali la kimantiki ni kwamba hao washiriki waliohojiwa ni wa mkoa gani?.

3.Utafiti umetaja viongozi wa UKAWA na namna wanavyokubalika. Je waliohojiwa wanatambulika misimamo yao juu ya uwepo wa UKAWA?.

4. Kuhusu wanasiasa waliotajwa kuwa na alama za juu. Swali ni kwamba idadi ya watu waliohojiwa kwa kila mkoa na itikadi zao zinafanana?. Ikiwa watu wamehojiwa Monduli unategemea nini?, au Babati tunategemea majibu gani, au Pemba tunadhani ni nani atapata alama za juu.

JUVICUF tunapongeza juhudi za TWAWEZA kuamua kufanya utafiti kuhusu hali ya kisiasa nchini, lakini sisi tunaamini siasa ya Tanzania hivi sasa imekua complex kutokana na Mazingira ya Kiuchumi na kijamii yaliopo nchini hivi sasa. TWAWEZA wangeweza kwenda mbali zaidi ya hapo walipofika kwa kuwafikia wananchi wengi zaidi na wenye mchanganyiko wastani wa kila aina ya makundi ya kijamii yaliopo nchini.
Watanzania Wataamua wenyewe mwakani kupitia masanduku ya Kura.

Imetolewa na Hamidu Bobali, Naibu Katibu Mtendaji JUVICUF.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments