NAMBA ZA SIMU ZA KIKWETE MAREKANI NA USALAMA WETU
Serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania iliwahi kutoa muongozo wa mawasiliano yote ya wafanyakazi wa serikali na idara zake nyingine kuhusu mawasiliano haswa ya barua pepe , simu na vifaa vingine vya serikali lakini agizo hili siku zote limepuuzwa na linaendelea kupuuzwa kila siku .
Ukisoma taarifa mbalimbali za ikulu kwa ajili ya umma utashangaa kukuta kuna anuani za barua pepe za google au yahoo ambazo kufungua ni bure kabisa tena hazionyeshi ni za mtu gani haswa , idara nyingine za serikali pia unakuta zina mawasiliano ya yahoo au mengine ambayo si ya serikali ya jamhuri lakini zinatumika kwenye mawasiliano ya nchi tena mengine ya siri kabisa kama mikataba na makubaliano mengine .
Siku za karibuni hapa watendaji hawa wa serikali wakatoa mpya wakati rais akiwa marekani anapata matibabu yake wakatoa namba ya simu ya marekani ili watu haswa watanzania wanaotaka kumjulia hali rais wao wafanye hivyo .
Kwenye suala hili kuna mambo ambayo tunaweza kuyajadili kwa upana kutokana na suala hili tata na pengine baadhi ya watu wanaohusika na mawasiliano wawajibike au wawajibishwe ndani ya idara zao wenyewe kutokana na taratibu zao za kazi .
Namba aliyotolewa ya kutuma ujumbe wa kumtakia kheri rais wa Tanzania ni +1-646-309-2295 hii ni namba ya marekani si namba ya Tanzania , kwahiyo mtu akituma ujumbe wake unahifadhiwa kwenye hifadhi huko marekani hata kama huku pia itahifadhiwa kwenye mtandao wa simu wa mtu husika .
Taarifa zinasema ni zaidi ya watu milioni 10 wametuma ujumbe mfupi yaani SMS kwenye namba hiyo kwa ajili kumpa pole rais na salamu nyingine zinazohusiana na rais , wengine wametuma ujumbe zaidi ya mara moja toka siku namba imetolewa hadharani .
Kama ni watu milioni 10 au zaidi na wametuma ujumbe kwenye namba ambayo iko marekani kwa usajili na kila kitu ina maana kuna kampuni moja duniani ambayo iko marekani imehifadhi namba za watanzania milioni 10 au zaidi tena bila taabu na bila makubaliano yoyote na watu husika .
Tujue idara ya usalama wa taifa ya marekani yaani NSA na shirika lao la ujasusi CIA ni watuhumiwa wakuu wa kudukua taarifa za mawasiliano ya watu kwenye nchi yao wenyewe nan chi nyingine mbalimbali duniani hata zile zilizoendelea sana ambazo zina mifumo imara ya ulinzi na wataalamu , hilo washauri wetu hawakuliona mpaka kutoa namba hiyo ya simu namba za watanzania zikusanywe ?
Kwanini watendaji wa ikulu wametoa namba ya nje tena marekani ambao ni watuhumiwa wa udukuzi wakati tuna kampuni ya simu yenye alama ya utaifa wetu Tanzania Telecommunications Company Limited yaani TTCL ? ambayo ingeweza kutoa namba za simu na huduma nyingine za mawasiliano kwa ajili ya shuguli hiyo na namba zikahifadhiwa na hao wenyewe TTCL na si mataifa mengine au kampuni nyingine ?
Hata kama hatuitaki TTCL kuna kampuni za mawasiliano kama TIGO , AIRTEL , ZANTEL , VODACOM , SMART , BOL na huduma nyingi za mawasiliano nchini ambazo zinaweza kutoa namba ya simu ambayo inaweza kutumika popote duniani katika kupiga , kupokea simu na shuguli nyingine za mawasiliano ?
Mbona kuna viongozi wengi wa nchi hii wanasafiri sehemu mbalimbali duniani kwa kutumia namba za simu za nyumbani na wanabaki na namba zao zile zile kwa ajili ya mawasiliano yao ya kila siku hili limeshindikanaje ?
Hili suala halikubaliki haswa kwa kiongozi mkubwa kama rais wa nchi , ni vizuri wahusika watoe ufafanuzi kuhusu suala hili na kama kuna watu wamezembea wachukuliwe hatua kali za kisheria ili iwe funzo wa watu wengine .
YONA FARES MARO
0786 806028
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments