[wanabidii] MSIMU WA KUWINDA PANYA MKOANI MBEYA

Saturday, November 15, 2014
MSIMU WA KUWINDA PANYA MKOANI MBEYA

Kama uko mkoani mbeya utaona kuna moto unawake mwenye milima miwili moja karibu na mjini na ule ulio karibu na stendi ya nane nane .

Moto uliowaka mwanzo maeneo ya mjini karibu na shule ya itiji tulifanikiwa kuuzima mimi na jamaa Fulani baada ya kujihada za masaa kadhaa siku ya leo .

Usiku huu naangalia tena naona wamewasha tena moto upande mwingine wa mlima na unawake kweli kweli .

Nilipowasiliana na wadau wakaniambia huu ni msimu wa kuwinda panya kwa ajili ya kitoweo , ule moto unafanya panya watoke kwenye mashimo kutokana na joto na mashimo yao kuonekana ili wawindaji waweze kuwashika .

Ukiacha hilo takwimu zinasema uchomaji moto ukiendelea hivi ifikapo mwaka 2017 kutakua na upungufu mkubwa wa maji na kama inavyojulikana watu wa huku wanategemea sana milima hiyo kama chanzo cha maji ya kutumia majumbani na kwa ajili ya kuoteshea mazao yao .

Hii dhambi ya kuchoma misitu , kuharibu vyanzo vya maji , kuharibu mazingira na hujuma nyingine itawarudia wenyewe miaka michache ijayo sijui watamkimbilia nani .

Suala la tabia nchi sio hadithi , tumeona na kusikia maeneo mengi watu wanapambana kati ya wafugaji na wakulima , sehemu nyingine ni vikundi vya waasi kama boko haram , hii yote ni kutokana na shida na dhambi zinazolelewa kama hizi .

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments