[wanabidii] Mkuu wa Mkoa aliyeachwa ashukuru; Atoa milioni 19/= za maabara

Sunday, November 16, 2014
Dk Ishengoma

BAADA ya kuachwa katika uteuzi wa wakuu wa mikoa, alisekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk Christine Ishengoma (pichani) amewaaga wakazi wa mkoa wa Iringa kwa kuchangia kiasi cha Tsh milioni 19 kwa ajili ya kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete la ujenzi wa maabara katika shule za sekondari.

Akizungumza katika mahojiano maalum na matukiodaima.co.tz leo, Dk Ishengoma ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum, mkoa wa Morogoro (CCM) alisema kuwa pamoja na kutemwa katika nafasi hiyo ya Ukuu wa Mkoa, bado anampongeza sana Rais Profesa Jakaya Kikwete kwa uteuzi wake kama Mkuu wa Mkoa, nafasi iliyoishia mapema mwezi huu baada ya Rais kuteua Wakuu wa Mikoa wapya wanne na kufanya mabadiliko kwa maadhi ya Wakuu wa Mikoa nchini, na Iringa nafasi yake kuteuliwa Bi Amina Juma Masenza.

Dk Ishengoma akifungua moja kati ya vikao vya RCC Iringa kulia ni mkuu wa wilaya ya Iringa Dr Laeticia Warioba
Dk Ishengoma alisema kuwa kabla ya uteuzi huo alikuwa akiendelea na utekelezaji wa majukumu yake mbali mbali ya kupigania maendeleo ya mkoa wa Iringa na kuwa siku moja kabla ya uteuzi huo alianza zoezi la kuhamasisa ujenzi wa maabara kwa kuanza kukabidhi mabati 150 katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa zoezi ambalo alikusudia kulifanya katika Halmashauri zote na fedha hizo za kununua mabati kiasi cha Tsh milioni 19 amelazimika kuzikabidhi kwa katibu tawala wa mkoa wa Iringa ili kuzikabidhi katika Halmashauri zilizosalia ikiwmo ya Iringa , Kilolo na Mufindi.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dk Ishengoma (wa tatu kulia walioketi) akiwa na baadhi ya wanahabari mkoa wa Iringa na viongozi wa wilaya ya Iringa na Manispaa ya Iringa katika moja kati ya vikao vyake na wanahabari Iringa

"kila waka nilikuwa nikiwasalimia kamwene ...makasi, hii ni kutokana na wakazi wa mkoa huu wa Iringa kupenda zaidi kazi .....niliupenda sana mkoa wa Iringa na watu wake jinsi ambavyo walivyo na moyo wa kujituma katika kazi sitausahau mkoa wa Iringa na nitaendelea kuusemia vizuri mkoa huu wenye historia kubwa nchini" alisema Dr Ishengoma
Dk Ishengoma (wa pili kulia) alipotembelea mabanda ya wakulima kuhamasisha kilimo

Kuwa akiwa mkoani Iringa amehamasisha ukuaji wa sekta ya utalii mikoa ya nyanda za juu kusini hasa mkoa wa Iringa kwa kuanzisha historia ya chifu Mkwawa na utunzaji wa kumbukumbu ya historia ya mkoa kwa kushirikianana chuo kikuu cha Iringa .
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (wa pili kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk Ishengoma (kushoto) wakati wa ziara yake Ludewa kabla ya mkoa wa Njombe kuzaliwa 

Pia kusimamia sekta ya Kilimo , ujenzi wa barabara na maji katika mji wa Iringa na maeneo mengine ila pia kuona mkoa wa Iringa unaondoka katika nafasi ya kwanza ya kuongoza katika maambukizi ya VVU nchini.

"Amini napenda sana kuwashukuru viongozi wote wa mkoa wa Iringa wakiwemo wa chama na serikali kwa kuonyesha ushirikiano ila nisingeweza fika mkoa wa Iringa kama mheshimiwa Rais hakuniteua hivyo nampongeza kwa kuniona na kuniteua ila bado ninayofuraha kubwa na maamuzi ya Rais kutoniteua na kusema atanipangia kazi nyingine kwa sasa nitaondoka kwenda mkoani kwangu Morogoro kuendelea na kazi ya ubunge "

Aidha aliwaomba wakazi wa mkoa wa Iringa kuendeleza ushirikiano wao kwa mkuu wa mkoa mpya Bi Amina Masenza pamoja na wakuu wa wilaya wote ili kuufanya mkoa huo kuzidi kupiga hatua katika nyanja ya kimaendeleo zaidi .



Katika uteuzi uliofanywa na Rais Kikwete Jumatano, Novemba 5, 2014 Wakuu wapya wa Mikoa walioteuliwa ni Bi. Halima Omari Dendego ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dkt. Ibrahim Hamisi Msengi ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Bi. Amina Juma Masenza ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Bwana John Mongella Vianney ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Taarifa inasema kuwa kabla ya uteuzi wake Bi. Dendego alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Dkt. Msengi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Bi. Masenza alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela na Bwana Mongella alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Aidha, taarifa hiyo ilisema kuwa Wakuu wa Mikoa ambao watapangiwa kazi nyingine ni Kanali (Mst) Fabian Massawe wa Kagera, Dkt. Christine Ishengoma wa Iringa na Kanali Joseph Simbakalia wa Mtwara.
Dk Ishengoma (wa kwanza kushoto) akiwa na mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda na Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abeid Kiponza siku walipotembelea Nduli kuhani msiba wa aliyekuwa diwani wa kata ya Nduli marehemu Chonanga 

Wakuu wa Mikoa ambao walihamishwa vituo vya kazi ni Bwana Magesa S. Mulongo ambaye alikwenda Mkoa wa Mwanza kutoka Arusha, Dkt. Rehema Nchimbi ambaye alikwenda Mkoa wa Njombe kutoka Dodoma, Bwana Ludovick John Mwananzila anakwenda Tabora kutoka Lindi, Kepteni (Mst) Anseri Msangi anayekwenda Mkoa wa Mara kutoka Njombe na Mhandisi Everist Ndikilo ambaye anakwenda Arusha kutoka Mwanza.

Wengine waliohamishwa ni Luteni (Mst) Chiku A.S. Galawa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutoka Tanga, Dkt. Rajab Rutengwe ambaye anakwenda Mkoa wa Tanga kutoka Katavi, Bi Fatma Mwasa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kutoka Tabora na Bwana Magalula S. Magalula ambaye anahamishiwa Lindi kutoka Geita.
Dk Ishengoma akimsikiliza kwa makini Katibu Msaidizi wa CCM mkoa Jimson Mhagama

Taarifa hiyo ilisema kuwa Wakuu wa Mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya,Morogoro, Pwani, Rukwa, Shinyanga, Ruvuma, Singida na Simiyu watabakia kwenye vituo vyao vya sasa.

Aidha, Rais Kikwete alifanya uteuzi wa Wakuu wapya wa Wilaya, kuhamisha baadhi yao na kutengua uteuzi wa baadhi.
Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma akiwa tayari kukabidhi vyeti kwa madereva boda boda mafunzo yaliyofadhiliwa na mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa Salim Asas (wa pili kushoto)

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments