[wanabidii] MKAKATI WA CHADEMA KWENYE UCHAGUZI MKUU WA 2015 KUPITIA UKAWA

Tuesday, November 18, 2014

JUU YA USHIRIKI WAKE KWENYE UCHAGUZI

 

UCHAGUZI MKUU WA 2015 KUPITIA UKAWA

 

 

UTANGULIZI:

 

Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ni mwamvuli wa kisiasa ulioasisiwa na vyama vitatu ambavyo ni Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Wananchi (CUF) na Chama cha NCCR Mageuzi. Baadaye chama cha NLD kimejiunga kwenye UKAWA na hivyo kufanya jumla ya vyama vinavyounda umoja huu kufikia vinne. Lengo la awali la mwamvuli huu lilikuwa ni kuwa na sauti ya pamoja katika kutetea na kusimamia Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya kama ilivyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba kwenye Bunge Maalum la Katiba tarehe 18 Machi 2014. Msukumo wa kutetea Rasimu hiyo umetokana na kubeba matakwa ya CHADEMA na CUF kuhusu muundo wa muungano ambapo Rasimu imependekeza muundo wa Serikali tatu ambao ndio pendekezo la vyama hivi. CHADEMA inaamini kuwa ikiwa muundo wa serikali tatu utapita, itakuwa ni rahisi kushinda uchaguzi wa Tanzania Bara ambako ina wafuasi wengi huku CUF nayo ikiwa na matumaini ya kushinda Zanzibar ambako imeota mizizi kutokana na sababu zinazofahamika. Kwa hali hiyo, hata kama CCM inaweza kushinda uchaguzi wa Muungano, hawatakuwa na mamlaka Zanzibar wala Tanzania Bara na hivyo kuwafanya wapotee kabisa kwenye siasa za Tanzania.

 

 

Baada ya jitihada za kutetea Rasimu hiyo kugonga mwamba kutokana na CCM kutuzidi ujanja na wingi wao bungeni ulitufanya tushindwe kwenye kila hatua ya bunge hilo, CHADEMA tumefanikiwa kubadili mwelekeo wa UKAWA na tumefanikiwa kushawishi vyama washirika kuendelea kubaki ndani ya mwamvuli wakati tukielekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Desemba 2014 na Uchaguzi Mkuu wa 2015. Kabla ya uchaguzi Mkuu, kutakuwa na Kura ya Maoni kupitisha Katiba inayopendekezwa ambayo tunaamini kuwa CCM watashinda. Hata hivyo, CHADEMA itaendelea kuwashawishi vyama vingine kuendelea kubaki ndani ya UKAWA kwa madai ya kupiga kampeni ya kura ya HAPANA ilhali CHADEMA ikitumia mwanya huo kujijenga kisiasa.

 

kwenye mchakato wa Katiba Mpya na hapana maoni UKAWA tutashindwa, nguvu kubwa ya CHADEMA kupitia mwamvuli wa UKAWA ni kwenye uchaguzi wa Serikali za

 

Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2015. Kwa mujibu wa Makubaliano ya UKAWA ambayo yalisainiwa tarehe 26 Oktoba 2014 kwenye viwanja vya Jangwani Dar es Salaam, vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR na NLD tumekubaliana kusimamisha wagombea wa pamoja kwenye nafasi zote. Mpango wa namna ya kuwapata wagombea ambao kwa kiasi kikubwa umeratibiwa na CHADEMA umekamilika na umesambazwa kwa vyama washirika. Hata hivyo, pamoja na makubaliano hayo, Mkakati wa CHADEMA ni kuhakikisha kuwa inasimamisha wagombea wengi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu kuliko vyama washirika wa UKAWA huku ikihakikisha kuwa nafasi ya mgombea Urais inaangukia kwa CHADEMA.

 


HALI YA KISIASA NDANI YA UKAWA KATIKA KIPINDI CHA KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NA UCHAGUZI MKUU

 

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika tarehe 14 Desemba 2014 na uchaguzi Mkuu umepangwa kufanyika Oktoba 2015 ambapo CHADEMA imekubaliana na vyama washirika wa UKAWA kusimamisha wagombea wa pamoja. Kikosi Kazi kilichoandaa mkakati huu kimetafakari kwa kina faida na hasara za maamuzi haya kwa CHADEMA kwa kuzingatia mazingira ya sasa na ya baadaye ya kisiasa ndani ya umoja huu. Kwa ujumla mambo yafuatayo yamebainika;

 

1.     Vyama vinavyounda UKAWA ni 'Regional and Tribal Based'. Chama cha NCCR Mageuzi kina wafuasi wengi Mkoa wa Kigoma tu. Hali hii inafanya chama hicho kuwa ni cha Kigoma na baadhi ya watu wanakiita kuwa ni chama cha Waha ijapokuwa kinaongozwa na Mwenyekiti asiye na asili ya Kigoma. Kwetu CHADEMA hii ni advantage kwani tutaweza kukidhibiti chama hicho kuenea katika mikoa mingine. CUF, ni chama kilichoshika hatamu kisiwani Pemba kutokana na sababu za kidini na historia ya Zanzibar. Kwa upande wa Tanzania bara, CUF imejipenyeza kwenye mikoa ambayo ina waumini wengi wa dini ya kiislam kama Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Tabora. Hii pia ni advantage ya CHADEMA kwani ukiondoa mikoa hiyo, CHADEMA ina nafasi ya kusambaa maeneo mengi na UKAWA kuongeza idadi tu ya vyama na kwa vile hawapo kwenye 'vita' ya kugombania

 

wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye chaguzi.

 

2.    Hali ya ndani ya CHADEMA bado haijakaa sawa baada ya maamuzi ya kuwavua uanachama Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba pamoja na maamuzi ya kumvua vyeo vyote ndani ya chama aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, ZITTO KABWE ambaye kwa sasa anaonekana kujiimarisha na kujizolea umaarufu kupitia sakata la ''ESCROW ACCOUNT''. Baadhi ya wafuasi wengi wa CHADEMA wamepoteza imani na chama na wengine wameamua kujiunga na chama kipya cha ACT huku wengine wakirejea CCM. Hali hii ni ishara mbaya na ina 'impact' kubwa kisiasa.

 

3.    Aliyekuwa mgombea wa CHADEMA kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, DK WILBROAD SLAA ameendelea kushuka umaarufu kisiasa kutokana na kuwa nje ya majukwaa ya kisiasa kwa muda mrefu. Hali hii inatokana na DK SLAA kutokuwa na nafasi yoyote ya kisiasa nje ya chama na hivyo kukosa fursa ya kushiriki mijadala ya kisiasa kama ile inayotokea bungeni. Aidha, umri wa DK SLAA ni kikwazo kikubwa kwake na kwa CHADEMA tunapoelekea mwaka 2015. Mwenyekiti wa CHADEMA, FREEMAN MBOWE licha ya kuwa kwenye uwanja wa siasa kwa muda mrefu kutokana na kuwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, hana sifa ya kugombea nafasi ya Urais kutokana na matakwa ya kikatiba hasa juu ya elimu ya mgombea. Suala la elimu limekuwa kikwazo kikubwa kwa MBOWE. Kwa upande Mwingine, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi na wa CUF, JAMES MBATIA na PROF IBRAHIM LIPUMBA ni changamoto kubwa kwa chama chetu wakati wa kupendekeza mgombea Urais. Kikwazo kikubwa kipo kwa Lipumba ambaye anaonekana anataka ateuliwe kugombea nafasi ya Urais kupitia UKAWA.

 

4.    Maadui zetu kisiasa, CCM wanaendelea kujiimarisha kisiasa na safu ya uongozi wa chama hicho imekuwa na mikakati imara kuliko ya CHADEMA na UKAWA kwa ujumla. Aidha, ziara anazofanya Katibu Mkuu wa CCM, ABDULRAHMAN KINANA na Katibu Mwenezi na Itikadi, NAPPE NNAUYE zimekuwa ni kikwazo kwetu katika kusambaza propaganda zetu katika maeneo ya vijijini. Pia Mwenyekiti wa CCM, JAKAYA KIKWETE amekuwa na mkakati imara wa kuhakikisha kuwa ahadi alizoahidi zinatekelezeka kabla hajamaliza muda wake hali ambayo imekuwa ni tishio kubwa kwa tumekuwa tukitumia udhaifu wa serikali kuleta kama mtaji wetu wa kudumu wa kisiasa.

 

5.     CHADEMA bado hakijajinasua na propaganda za wapinzani wetu kuwa ni chama cha Wachagga na Wakristo ijapokuwa ina wabunge katika baadhi ya miji mikuu ya mikoa kama Mbeya, Iringa na Arusha. Mabadiliko ya kiuongozi mathalan kwa kumweka Prof ABDALLA SAFARI kuwa Makamu Mwenyekiti nafasi ambayo ilichukuliwa na SAID ARFI bado hayajafuta dhana hiyo kwani hakuna mabadiliko yoyote makubwa yaliyofanyika kwa nafasi za Mwenyekiti na Katibu Mkuu.

 

6.     CHADEMA haina mizizi mikubwa vijijini ambako ndiko waliko wapiga kura wengi.

 

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo Kikosi Kazi imeyabaini ambayo ni changamoto kubwa kwa chama chetu tunapoelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2015. Ili kukabiliana naa changamoto hizo, Kikosi Kazi kinapendekeza mambo yafuatayo;

 

a.     CHADEMA kiendelee kuwa 'chama kiongozi' ndani ya UKAWA. Njia rahisi ya kuendelea kuwa chama kiongozi ni kwa kufadhili harakati na shughuli muhimu za UKAWA kutokana na CHADEMA kuwa na vyanzo vingi vya ndani na nje ya nchi ambavyo vinaweza kutumika kugharamia shughuli za UKAWA na hivyo kukifanya CHADEMA kuwa na sauti KUU.

 

b.     Viongozi wakuu wa CHADEMA, Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Mwenyekiti wa BAVICHA, BAWACHA na Baraza la Wazee wafanye ziara zisizokatika mikoani kwa lengo la kuinadi UKAWA huku msukumo mkubwa ukiwa kukitangaza CHADEMA. Katika mikutano hiyo, Viongozi hao waendelee kutumia kauli mbiu ya Peoples Power na vionjo mbalimbali vya chama kama Kunja Ngumi ili kuwafanya wanaohudhuria mikotano hiyo wajenge taswira ya CHADEMA zaidi kuliko UKAWA. Mkazo mkubwa wa mikutano hiyo uwe kwenye mikoa ambayo CHADEMA ina wafuasi wachache kama vile Kigoma, Lindi, Mtwara, mikoa ya Kanda ya Kati na Mikoa ya Kanda ya Ziwa.

 

c.      Lipumba na Mbatia washauriwe kugombea ubunge badala ya urais. Hali hiyo itafanya CHADEMA kuwa na nafasi kubwa ya kuteua mgombea urais wa UKAWA na bila shaka DK SLAA anaweza kuendelea kuwa mgombea Urais licha ya mapungufu yaliyobainishwa. Juhudi zilizofanywa za agombee jimbo la Vunjo na Lipumba agombee kwa vile ndio njia pekee ya kuviondoa vyama

 

hivyo kwenye kinyang'anyiro cha Urais 2015.

 

d.    CHADEMA kihakikishe kuwa kinashawishi vyama vingine vya UKAWA visisimamishe wagombea kwa baadhi ya maeneo yenye wafuasi wao wengi. Mathalan, kwa vile NCCR inakubalika zaidi Kigoma, CHADEMA ishawishi NCCR kugawana majimbo kwa uwiano unaoleta faida kwa Chama na vyama vyote washirika viwashawishi wanachama na wafuasi wao kuwapigia kura wagombea wa CHADEMA. Hali hiyo ijitokeze pia kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Wakati huo huo, CHADEMA ihakikishe kuwa inasimamisha wagombea wengi katika maeneo inayokubalika na isikubali kutoa mwanya kwa vyama vingine kusimamisha wagombea labda kwa maeneo machache ambayo hayatakuwa na athari kwa chama.

 

e.     CHADEMA itumie UKAWA kujiimarisha vijijini hasa katika maeneo ambayo haikubaliki kama vile Lindi Mtwara, Dodoma nk.

 

f.      Midahalo ya kisiasa ya kukijenga chama ifanyike mara kwa mara na irushwe kwenye vituo vya Runinga hususan ITV ambayo tuna mkataba nayo mahsusi na tunapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa mmiliki.

 

g.     hamasa kwenye mitandao ya kijamii iendelee kuwekwa na Kikosi Kazi mitandaoni kiimarishwe kutokana na sasa kupata upinzani mkubwa kutoka kwa vijana wa CCM ambao wanajulikana kama Lumumba Buku Saba au LB7.

 

h.    Viongozi wa CHADEMA wajiepushe kushiriki kwenye mijadala inayojenga wapinzani wetu kisiasa. Hoja kama ya ESCROW ACCOUNT kwa vile haijaasisiwa na Viongozi watiifu wa CHADEMA isiwapoteze muda wa kukijenga chama kwani kujiingiza kwenye mijadala ya hoja hiyo ni kuwapa umaarufu Kafulila na Zitto ambao wote wamepitia CHADEMA.

 

i.       CHADEMA itumie UKAWA kupata misaada zaidi ya kifedha. Kwa kuwa wafadhili wa nje wameonekana kuunga mkono UKAWA, CHADEMA kiendelee na mikakati ya kubuni mambo ambayo yatasaidia kujipatia mapato kwa mgongo wa UKAWA. Aidha, harambee za ndani ziendelee kufanyika kwa mgongo wa UKAWA.

 

 zo yaliyomo kwenye Mkakati Huu. Kikosi Kazi kati na kwa kuzingatia hadidu rejea tulizopewa.

 

Hakika haikuwa kazi rahisi na yaliyomo kwenye Mkakati Huu mengine hayafurahishi. Hata hivyo kwa vile lengo ni kukijenga chama, Kikosi Kazi kinaamini kuwa ukakasi uliojitokeza ni katika kutafuta tiba mbadala. Kwa vile mkakati huu ni wa siri, ni matumaini ya Kikosi Kazi kuwa utaendelea kuwa siri na utawafikia viongozi wakuu tu wa CHADEMA ambao ndio wenye mamlaka ya kuratibu na kusimamia harakati za chama ndani ya UKAWA. Kuvuja kwa mkakati huu ni mwanzo wa siasa za kutoaminiana ndani ya UKAWA. Taarifa kamili ya mkakati huu imeambatishwa na muhtasari huu.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

Previous
Next Post »
0 Comments