[wanabidii] Fwd: [New post] Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema “Hatutetereki”

Wednesday, November 12, 2014
-------- Original Message --------
Subject: Fwd: [New post] Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema "Hatutetereki"
From: ibrahimu ngupula <ibrangupula@gmail.com>
To: Godfrey Ngupula <ngupula@yahoo.co.uk>,paul kiyumbi <pxkiyumbi@gmail.com>,RICHARD KAIZA <rwegasila@gmail.com>
CC:

---------- Forwarded message ----------
From: Zitto na Demokrasia <comment-reply@wordpress.com>
Date: Sun, 9 Nov 2014 10:07:53 +0000
Subject: [New post] Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema "Hatutetereki"
To: ibrangupula@gmail.com

Post : Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema
"Hatutetereki"
URL : http://zittokabwe.wordpress.com/2014/11/09/nashambuliwa-tunashambuliwa-pac-tunasema-hatutetereki/
Posted : November 9, 2014 at 1:07 PM
Author : zittokabwe
Tags : eSCROW ACCOUNT, Harbinder Singh Seth, Independent Power
Tanzania Ltd (IPTL), IPTL, PAC, Zitto Kabwe
Categories : Uncategorized

Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema "Hatutetereki"

Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya Kamati ninayoongoza ya PAC
kuwasilisha Bungeni Taarifa Maalumu kuhusu ukaguzi maalumu wa akaunti
ya Tegeta Escrow, kumekuwa na kampeni za chini chini zinazoendeshwa
kwenye korido za Bunge na kwenye mitandao dhidi yangu binafsi na
baadhi ya wabunge waliosimama kidete dhidi ya wizi wa fedha kutoka
Benki Kuu ya Tanzania akaunti ya Escrow.

Baadhi ya tuhuma nimezipeleka kwenye vyombo vya dola ili zichunguzwe
kwani zina vielelezo vya mahala pa kuanzia (kama leseni ya udereva ya
mwanamke anajulikana kama Vivian Emmanuel Sirikwa na muhuri wa kampuni
ya uwakili inayomilikiwa na Bwana Joseph Mkandege).

https://zittokabwe.files.wordpress.com/2014/11/vivian.jpg&h=300

Baadhi ya tuhuma nitazijibu moja baada ya moja.

Waziri mmoja ambaye ni mtuhumiwa wa wizi wa fedha za Tegeta Escrow
anazunguka kwa wabunge akisema tuhuma hizi kupikwa kama njia yake ya
kuhamisha mjadala kutoka uporaji wa Tshs 200 bilioni kwenda kwenye
masuala binafsi.

Tuhuma hizi zenye kichwa cha habari "Zitto na Filikunjombe wanatumiwa
na Kenya na Uingereza kuvuruga na kudhoofisha Uwekezaji nchini mwetu"
zinajibiwa hapa chini. Utaona ndugu Filikunjombe ametajwa kwa kichwa
cha habari ili kumtaja tu bila sababu yeyote ile.

Tuhuma #1:

Zitto anaye rafiki yake Mkenya aitwae Rapahel Ongangi ambao kwa pamoja
wameanzisha Gombe Advisors Co. Ltd (registered on 24 November 2011,
Certificate No 87387) kwa ajili ya kufanya biashara na Makampuni ya
Gesi na Mafuta yanayofanya kazi nchini hapa.

Majibu:

Gombe Advisors ni kampuni binafsi isiyofanya faida yaani 'Company
Limited by Guarantee'. Haina kazi na kampuni yoyote ya Gesi na Mafuta
na wala yenyewe haijuhusishi na biashara hiyo. Gombe advisors
haijafanya kazi yoyote ile na kampuni nyingine zaidi ya kusaidia
wasanii wa kundi la Kigoma All stars. Upotoshaji hapa unalenga
kupindisha mjadala.

Tuhuma #2:

Zitto amemsaidia Ongangi kupata uraia wa Tanzania na kwa sasa ni raia
wa pasipoti. Zitto na Ongangi walimtafutia CEO wa Shell aitwae Axel
Knospe nyumba na gari ya kukodi.

Majibu:

Raphael ni mtu binafsi ambaye anafanya shughuli zake hapa nchini,
amesoma hapa nchini na ameoa na ana mtoto. Tuhuma hizi hazina msingi
wowote ule maana ni uwongo. Wanaotoa tuhuma hizi waonyeshe hiyo
pasipoti ya Bwana Ongangi kuthibitisha madai yao.

Tuhuma #3:

Mikataba ya STATOIL iliyokuwa inarushwa kwenye mitandao ya jamii na
kuchapishwa kwenye magazeti ya Kenya ya hapa nchini (The Citizen na
Mwananchi) mwandishi mkuu alikuwa huyo CEO wa Shell.

Majibu:

Mkataba uliovujishwa wa StatOil ulivujishwa na waandishi wa habari wa
Norway. Uchambuzi wa mkataba huo nimeufanya mwenyewe kwa kutumia
utaalamu wangu niliosomea wa kuchambua mifumo ya kodi kwenye sekta ya
mafuta na gesi. Kwa namna yoyote ile, huyo anayetajwa kuwa CEO wa
kampuni ya Shell hahusiki. Tuhuma hii wanaoitoa watoe ushahidi usio na
chembe ya mashaka.

Ikumbukwe kuwa mkataba wa StatOil utaipotezea Tanzania mapato ya dola
za Marekani bilioni 12 (takribani Tshs 20,400,000,000,000/=) katika
kipindi cha miaka 15 baada ya gesi kuanza kuchimbwa.

Uamuzi wa Kamati ya PAC kutaka mikataba yote ya Gesi kuwa wazi una
lengo la kuchambua kuona kama mikataba yote nchini haipotezi mapato
kwa nchi. Uamuzi huo umewakasirisha sana baadhi ya waliohusika kuingia
mikataba Serikalini maana wanajua kuna madudu kwenye mikataba na
wanataka umma wa watanzania usijue!

Tuhuma #4:

Kampuni ya SHELL imechukizwa sana kucheleweshwa kwa kupata kibali cha
kutafuta gesi na mafuta kule Pemba. Vilevile SHELL haina uwekezaji
mkubwa Tanzania Bara kwani ilishindwa kwenye tenda zenye vitalu vyenye
gesi nyingi upande wa Bara.

Majibu:

Ukweli ni kuwa Kampuni ya Shell ina vitalu 4 huko Zanzibar na tayari
ina makubaliano na Serikali ya Zanzibar kuhusu utafutaji mafuta huko
katika vitalu namba 9,10,11 na 12. Shell inafanya kazi na kampuni ya
Petrobras ya Brazil kwenye kitalu namba 6 na namba 8. Taarifa hizi
zipo wazi kwenye tovuti ya TPDC. Tuhuma nyepesi namna hii dhidi ya
kampuni kubwa kama Shell zinaonyesha dharau na kiburi kinachotokana na
uelewa mdogo wa mambo wa watu wanaotuhumu.

Tuhuma 5:

Ongangi anapokea maelekezo kutoka Serikali ya Kenya kuhujumu uwekezaji
nchini mwetu.

Majibu:

Nazifahamu mbinu nyingi zinazotumika kufanya propaganda, lakini mbinu
hii imeshindwa ikiwa mapema sana. Ni vema wanaotoa tuhuma hizi
wazithibitishe vinginevyo ni mwendelezo wa propaganda zisozingatia
diplomasia ndani yake dhidi ya jirani zetu wa Kenya. Hizi ni
propaganda hatari ambazo hata hao wanaotuhumiwa wakisikia watatudharau
sana.

Tuhuma #6 (juu ya Uingereza):

Uingereza imekuwa inamfadhili Zitto kwa miaka mingi kwa mambo yake ya
kisiasa kwa hiyo sasa hivi Ubalozi wa Uingereza unamlipa Zitto na
Kafulila kuhakikisha kwamba Standard Chartered ya Uingereza inalipwa
deni lake lisilotambulika kisheria nchini mwetu.

Majibu:

Nimetangulia kusema hapo awali kuwa kuna propaganda ambazo haziangalii
hata diplomasia; nyingine ni hii. Pamoja na kukanusha uzushi huu, ni
vizuri wanaotoa tuhuma za namna hii kuthibitisha. Mimi binafsi
sijawahi kufadhiliwa kisiasa na Taifa lolote lile. Inaelekea kuna
wanasiasa wanaofadhiliwa na mataifa mengine ambao kwakuwa kwao ndiyo
maisha wanaamini na wengine tupo kama walivyo.

Kwangu itikadi yangu ni 'Uzalendo kwa nchi yangu', ni jambo ambalo
halina mbadala wake. Siku zote nasema "Right or wrong, my country
first".

Kurudia kurusha tuhuma kwa Ubalozi wa Uingereza nchini ni kudhihirisha
kwa mara nyingine kiburi cha kuwa na mamlaka (arrogance of power)
walicho nacho wanaotuma tuhuma hizi.

Aidha, wanatuhumu kuwa "Kafulila na Zitto wamehaidiwa 15% ya USD 150
million kama deni likilipwa"

Mtanzania anayeweza propaganda dhaifu kama hizi basi anatakiwa
ajitafakari. Hata hivyo ni vema wanaotoa tuhuma hizi wathibitishe bila
chembe ya mashaka.

Tuhuma #7:

Mbunge Mkono nae ameshikwa hasira kupoteza kazi ya uwakili pale
TANESCO. Kafulila na Zitto wanalipwa na Mkono kuvuruga Serikali kwa
hasira za kukosa fedha za kitapeli za TANESCO.

Majibu:

Hizi ni tuhuma ambazo sasa tumezizoea kutolewa. Mambo mepesi hayawezi
kujibu mambo ya msingi kama tuhuma za wizi wa fedha zaidi ya Tshs
bilioni 200 kutoka Benki kuu ya Tanzania. Kukusanya kila propaganda
ili kuuhamisha umma ni kupungukiwa hekima na busara.

Aidha, wanaotuhumu wanadokeza kuwa "Naomba tuwe macho na Wabunge wetu
achananeni na madai ya Zitto ya wizi. Huyu mtu anafanya biashara na
Kampuni ya SHELL na inasemekana analipwa na Ubalozi wa Uingereza.
Serikali ya Kenya na tapeli mkubwa Mbunge Mkono nae anawalipa Zitto na
Kafulila".

Watanzania, haya ni maneno ya hasira ya watu wanaokaribia kukamatwa
kwa kushiriki wizi wa fedha katika Benki kuu ya Tanzania. Kamwe tuhuma
kama hizi haziwezi kutukatisha tamaa katika kupambana ili ukweli
ujulikane. Sisi tutapigana kwa ajili ya Taifa, kwa ajili ya mtanzania
na tunachotaka ni umma uujue ukweli wa mambo.

Hasira hizi zinatokana na mambo mawili:

Moja ni uamuzi wa kamati ya PAC kuwasweka ndani baadhi ya watendaji wa
TPDC kwa kushindwa kutekeleza maamuzi ya Kamati yanayohusu uwazi wa
mikataba ya Gesi na Mafuta.

Pili, ni uamuzi wa PAC kuagiza ukaguzi maalumu wa mchakato mzima wa
kuanzishwa na kufungwa kwa akaunti ya Tegeta Escrow ambapo zaidi ya
shilingi bilioni 200 ziliporwa na zaidi ya shilingi bilioni 12
zinalipwa na TANESCO kila mwezi kwenda kampuni ya PAP inayomilikiwa na
Harbinder Singh Seth (50%) na watu wasiojulikana kupitia kampuni ya
Simba Trust iliyosajiliwa na kufichwa nchini Australia (50%).

Ieleweke kuwa PAP inalipwa shilingi milioni 400 kila siku kutoka
TANESCO izalishe au isizalishe Umeme! Watanzania, PAP itaendelea
kulipwa namna hiyo kwa miaka 20 ijayo. Kwa namna ambayo Seth analindwa
na baadhi ya watendaji Serikalini na hasa ndani ya Wizara ya Nishati
na Madini. Aidha, kuna fununu kuwa kuna maofisa serikalini wanaomiliki
hizo 50% za kampuni ya PAP. Seth pia anamiliki kitalu cha gesi Mnazi
bay Kaskazini kupitia kampuni ya HydroTanz.

Hasira hizi walizo nazo wanaonituhumu na Kamati yangu zimewapelekea
kugushi nyaraka mbalimbali zinazonituhumu mimi na wenzangu ili
kutuogopesha na kutukatisha tamaa katika kutafuta ukweli juu ya suala
la uporaji wa fedha kutoka Benki kuu. Lengo lao ni kututoa kwenye
mstari. Mimi na wenzangu hatutatoka kwenye mstari, tutashirikiana na
wabunge wenzetu kuhakikisha ukweli unajulikana na wezi kuchukuliwa
hatua kali.

Harbinder Singh Seth aliiangusha Serikali ya KANU nchini Kenya, sasa
anachotaka kukifanya kinaweza kuiangusha Serikali ya CCM wakiendelea
kumkumbatia.

Watanzania sio mabwege!

Zitto Kabwe

Mwenyekiti PAC

Dodoma, 9 Novemba 2014

Add a comment to this post:
http://zittokabwe.wordpress.com/2014/11/09/nashambuliwa-tunashambuliwa-pac-tunasema-hatutetereki/#respond

--
WordPress.com | Thanks for flying with WordPress!

Manage Subscriptions
https://subscribe.wordpress.com/?key=ffe6a63a21b70bdfe19aee993b6cce44&email=ibrangupula%40gmail.com

Unsubscribe:
https://subscribe.wordpress.com/?key=ffe6a63a21b70bdfe19aee993b6cce44&email=ibrangupula%40gmail.com&b=DDaQ-%5BwD%2518.%2FA0mCMT9MnU51z%5DPWPn%3F.lxyF%2F%5DovF39jvkGS%25

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments