Sent from my iPad
Begin forwarded message:
From: Muhammedkhatib <muhammedkhatib@yahoo.co.uk>
Date: 21 Novemba 2014 11:39:52 alasiri GMT +03:00
To: Mzalendo <mzalendonews@yahoo.com>
Subject: Mapiku
Mapiku
(Dr.Muhammed Seif Khatib)
Michezo ipo mingi duniani.Ipo ya kukikmbia na kuruka.Ipo ya kutumia viungo
vya mwili na vifaa vya michezo.Wakati mwengine hutumika vyote viungo
vya mwili na vifaa vya michezo.Ipo michezo ya majini na nchi kavu.ipo ya
ya binadamu kucheza na wanyama,samaki,nyoka na wadudu.Mwanadamu katu hakutindikiwa katika michezo.Ipo iliyochezwa ikazoeleka na sasa haipo
imesahaulika.Ipo inoshika kasi na kuendelea.Lakini ipo mingi sana itakayobuniwa na kuhuishwa.Hakuna kiumbe mwenye hati miliki ya michezo.
Katika michezo iitwayo michezo ambayo kwangu nashindwa kuitafsiri kuwa
ni michezo pamoja na ndondi au wengine huyaita masumbwi na mieleka.Katika
ngumi watu wawili wanatafutwa au wanatafutana.Watu hawa hawana ugomvi
wa asili na wala kisa!Wanakutanishwa baada ya kila mmoja kuiiandaa kwa
namna bora ya kumtwanga mwenzake kwa haraka na wepesi.Wanapandishwa
juu ya jukwaa la wazi.Kamba zinafungwa pembeni ili yeyote kati yao asikimbiye.Kabla ya 'mchezo' kuanza kila mmoja kati yao anajazwa mori
na jazba akisikia tu kengele,hakuna msaliye mtume- ni kumvurumishia mwenzako
mvua ya masumbwi mtawalia hadi mmojawapo adondoke au azirai.Na nasikia
hata ikitokea mmojawapo akauwawa,hakuna kesi.Kisa?walikuwa eti wote
mchezoni.Hawa hawatafautiani na ile mijitu ya mireka.Hupambanishwa,
hupiganishwa na hubiringanishwa kama mafahali ya vifaru.Nasikia hata wao
ukivunjwa shingo au kiuno, hakuna kesi ya kujibu.Kisa?walikuwa michezoni.Lo
masalale!Hata hivyo Waswahili wana michezo ya kitako.Hawavunjani viuno
wala kunyongana shingo.Hucheza dhumna,bao au karata.Alasiri au usiku katika majamvi,busati au mikeka huketi.Wakiwa na misuri,seruni,kanzu na
kofia za viua zilodenguliwa huifurahia michezo hiyo.Katika karata huwepo
michezo anuwai.Upo mchezo uitwao'Wahedi ustini' yaani sitini na moja.
Mwengine 'jore' na 'Chanisi' na pia upo wa 'Mapiku'.Idadi ya karata hizi 52 huwa alama zake na rangi zaka ambazo zinajitafautisha na maana maalum
katika kila mchezo.Rangi muhimu ni nyekundu,kijani,nyeusi na manjano.Chapa
au alama za karata ni shupaza(jembe),kopa(moyo) kisu na mavi ya mbuzi.Zile
zenye picha hupewa majina kadha Malikia, Mfalme au Basha!Uchezaji wa karata hutaka ujuzi,busara na hekima ingawa ni mchezo.Mchezo wa mapiku
hauna turufu maalum.Karata kubwa huila ndogo.Wajuao kuusoma mchezo na
mbinu huweza kuendesha kapa katika kila mchezo. Mchezo wa siasa wa
Tanzania kati ya chama cha mapinduzi na vyama vikuu vya upinzani ni sawa
na karata za mapiku.Kila karata za siasa zikichanganywa Chama cha
Mapinduzi kinavipiku vyama vya upinzani na kuviendesha ama mrisi au
kapa. Unajua kwa nini?Chama cha Mapinduzi kinajipanga hakikurupuki.Mfano
mzuri ni mwenendo wa Bunge la Katiba lililopita.Wapinzani wakiendeshwa
na genge la wanaharakati bila kufikiri,bila kupima na bila malengo wakafutuka
na kitimka bungeni.Ukiuliza hoja gani ya msingi,huoni.Wakiwa nje ya Bunge
kwa mtindo uleule wa jazba na munkari wakatangaza wataandamana kwa
nchi nzima bila kibali.Wataendesha migomo ya nchi nzima bila shurti na
watafanya mikutano nchi nzima bila kibali.Jazba za wanaharakati hawa
zikafifia hivi hivi na wao kunyamaza.Wakawatuma baadhi ya waandishi wa
habari wapeleka hoja mahakamani kuhoji uhalali wa Bunge la Katiba.Wakiwa
nje ya mahakama wakawa na matumaini kuwa Bunge litasimamishwa.Hoja
yao ikauwawa siku ya kwanza.Wakawageukia baadhi ya eajumbe wa Tume
ya Kukusanya maoni huku wakitumia Taasisi ya Mwalimu kinyume na
matakwa yake kuhoji jambo alilokuwa analipigania katika uhai wake wote.Nayo taasisi hiyo imejiaibisha katika hadhira ya Tanzania.Wanaharakati
hawa wanaojidhani wanasiasa wakamvamia Rais Kikwete kumtaka yale
mambo ya msingi yarekebishwe katika katiba ya zamani endapo thuluthi
mbili za kila upande, bara na zanzibar, hazipatikani.Mwanasiasa Rais na
wanaharakati wa kambi ya upinzani wakasubiri.Tamaa ya fisi ikawatoa
roho.Rais akawkubalia mambo kadha yakiwemo; Tume Huru Ya Uchaguzi,
Mshindi apate zaidi ya nusu ya kura zote za Urais,Matokeo ya Urais yeweze
kuhijiwa mahakamani,Mgombea Binafsi akubaliwe na kadhalika.Wanaharakati
wakaamini kuwa Zanzibar nawawezi kipata thuluthi mbili.Matokeo na ndoto
zao hazikuwa.Thuluthi mbili zimepatikana.Aidha yale maombi yao yote
yakawemo katika Katiba inayopendekezwa.Wanaharakati hawaamini
nini kimetokea!Wapo njia panda.Maombi yao yote yameingizwa katika katiba
inayopendekezwa.Kwa mantiki wanapaswa wende kwa Rais na kumshukuru
kwa kuwashawishi wabunge wake na waitifaki wake kukubali kuingiza
mambo yao yote waliyoyapigania.Ile lugha ya kuwa katiba imechakachuliwa
ya wanaharakati haina uzito tena.Munkari na jaziba iliyotia fora ni ya
kutangaza umma kuwa uchaguzi wa vijiji,mitaa na vigongoji mchakato wake
ukianza watasimamisha mgombea mmoja kwa niaba ya vyama vinne.Labda
ni mapema kuona kama hili limetendeka.Kwa vyovyote busara na hekima za
viongozi wa chama cha mapinduzi zimekuwa daima zinawapiku genge la
wanaharakati wanaojidhani kuwa ni wanasiasa.Hivi wanaposhindewa
katika chaguzi dhidi ya chama cha mapinduzi wanaweza kuijitetea kwa
hoja gani?Kutofaulo kwa kila jambo lao katika uwanja wa siasa ni nani
alaumiwe?Kila mchezo una mbinu na matao yake.Mchezo wa siasa wa
karata wa mapiku hautaki wanaharakati unawataka wanasiasa kwa
wanasiasa.Chama cha Mapinduzi kinajua mchezo wa mapiku ndio maana
kila siku kinawapiku vyama vya upinzani.
Oo
Sent from my iPad
0 Comments