Re: [wanabidii] USAJILI WA MAKANISA NA HUDUMA MBALIMBALI

Tuesday, November 11, 2014
Asante Yona kwa taarifa nzuri. Nimesikia kuwa tangu 2005 hadi 2014 ni makanisa 3 tu yameandikishwa baada ya uandikishwaji kuhamishwa toka wizara ya mambo ya ndani hadi ikulu. Sijapata taarifa kuwa ni misikiti mingapi imeandikiswa. You are a researcher, what do you have to say about this claim? Mimi nimehamishwa na andiko lako kuuliza maana huwa unafanya utafiti katika undikaji wako. Any comment?


On Monday, 10 November 2014, 18:40, Yona Fares Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:


USAJILI WA MAKANISA NA HUDUMA MBALIMBALI
JIBU LA MAISHJA - 09/11/2014 - UKURASA 4
Makanisa na huduma mbalimbali zote zinasajiliwa katika ofisi za wizara ya mambo ya ndani. Hakuna utofauti mkubwa katika taratibu za usajili kati ya shirika au chama cha kijamii na taratibu za usajili wa kanisa au huduma. Kitu kikubwa ambacho kinaweza kuwa kinatofautiana ni Muundo wa Katiba ya Kanisa au Huduma hiyo. Ili kufanikiwa kusajili kanisa au huduma unahitaji vitu vifuatavyo:-
i Katiba; zitahitajika ziandaliwe nakala za katiba kulingana na uhitaji uliopo. Kwa kuwa katiba hiyo yaweza kuhitajika katika ngazi ya kata na wilaya kabla ya kwenda wizara ya mambo ya ndani, ni vyema zikaandaliwa nakala tano au zaidi. Mwishoni zinatakiwa zibaki nakala 3 za katiba hiyo ambazo zitapelekwa Wizara ya Mambo ya Ndani kwa ajili ya kuwasilisha maombi ya usajili wa shirika lenu.
ii Fomu; Mtapaswa kujaza fomu mbili yaani SA. 1 na SA. 2 na kutoa nakala nyingine mbili za fomu hizo. Fomu hizo zinapatikana katika ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani – kitengo cha usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali. Katika fomu hizo mtahitajika kujaza taarifa mbali mbali ikiwemo; Jina la shirika, Mahali ofisi za shirika zilipo au zitakapokuwepo, anwani ya shirika, madhumuni ya shirika, sahihi za viongozi (fomu SA. 1). Taarifa nyingine ni pamoja na, kama shirika lina ushirikiano wowote au ni tawi la shirika jingine lolote la kitaifa au kimataifa, aina ya wanachama wa shirika, idadi kamili ya wanachama wa shirika, tarehe shirika lilipoanzishwa, wilaya ipi ambayo shirika linaendesha shughuli zake, kama shirika lina ardhi yoyote, vyeo vya viongozi na muda wao wa kukaaa madarakani, na sahihi za viongozi (fomu SA. 2).
iii Muhtahsari wa Kikao cha Waanzilishi wa Kanisa au Huduma; Muhtahsari wa kikao cha waanzilishi wa kanisa au huduma ni muhimu sana. Muhtahsari huu ndio utakaoonyesha kwamba kikao kilikaa na kuamua kuanzisha kanisa hilo, kuteua viongozi wa kanisa pamoja na kupitisha rasimu ya katiba ya kanisa hilo. Muhtahsari wa kikao unapaswa uonyeshe mahudhurio ya wajumbe wote wa kikao na kila aliyehudhuria kikao hicho anapaswa kusaini kuonyesha kuwa amehudhuria kikao hicho.
iv Orodha ya Waasisi; Orodha ya waasisi ni muhimu sana inaweza kuwa peke yake au ikaambatishwa pamoja na muhtahsari wa kikao. Wanachama hawa waanzilishi hawapaswi kuwa chini ya 10, bali wanapaswa kuwa 10 au zaidi.
v Wasifu wa Viongozi wa Shirika na Picha Zao; Mnapaswa pia kuandaa wasifu wa viongozi wa kanisa (CV) pamoja na picha zao (passport size). Wasifu huo wa kila kiongozi unapaswa kuwa nakala 2 au zaidi kulingana na uhitaji uliopo. Wasifu wa viongozi unapaswa kutoa taarifa muhimu za kiongozi ikiwa ni pamoja na, jina, tarehe ya kuzaliwa, mahali pa kuzaliwa, taarifa ya ndoa, anwani kamili, elimu, uzoefu wa kazi na mambo mengine muhimu. 
vi Barua ya Kuungwa Mkono/Utambulisho; barua ya utambulisho inapaswa kutoka kwa mkuu wa wilaya ambayo ofisi ya kanisa hilo ilipo. Mara nyingi barua hii inapatikana baada ya kupata utambulisho kutoka ngazi ya mtaa au kata kwenda katika ofisi ya mkuu wa wilaya. Kwa upande mwingine unaweza kupata barua ya utambulisho kutoka kwa uongozi wa huduma au kanisa jingine au kutoka katika ofisi za Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste (PCT), Jumuiya ya Kikristo ya Tanzania (CCT), Baraza la Maaskofu wa Katoliki Tanzania (TEC).
vii Barua ya Maombi ya usajili kutoka kwa Uongozi wa Kanisa; Barua ya maombi ya usajili kutoka kwa uongozi wa kanisa ni muhimu sana kwa kuwa ndio inayowasilisha maombi ya shirika katika ofisi za wizara ili lianze mchakato wa kushughulikia usajili wa shirika hilo.
viii Ada ya usajili; ada ya usajili inalipiwa katika ofisi za wizara ili kusaidia mchakato wa usajili upate kuendelea. Ada imegawanyika katika mafungu mbalimbali ikiwemo; ada ya maombi ya usajili, ada ya usajili, ada ya kila mwaka baada ya kusajiliwa pamoja na gharama nyinginezo. Ni muhimu kupata taarifa sahihi kutoka kwenye ofisi hizo juu ya gharama zipi mnapaswa kulipa.
Mara baada ya kujiridhisha kuwa nyaraka zote muhimu zimepatikana ikiwa ni pamoja na Ada ya usajili unaweza kupeleka nyaraka zako katika Ofisi ya Msajili iliyopo katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Kitengo cha Usajili wa Vyama vya Kijamii, Makanisa na Huduma mbalimbali. Ofisi ikishapokea maombi yako na malipo ya ada ya usajili itaendelea na utaratibu wa kusajili shirika hilo. Ili kuthibitisha usajili wa kanisa hilo ofisi hiyo itatoa cheti cha usajili wa kanisa hilo. Mara baada ya kupata usajili ni muhimu kuzingatia kwamba, kanisa linapaswa kupeleka ripoti ya utendaji na fedha ya kila mwaka katika ofisi hizo ikiwa ni pamoja na kulipia ada na tozo mbalimbali mnazopaswa kulipa kila mwaka.
Ni muhimu pia kuzingatia kwamba, madhehebu au huduma huwa na baraza la wadhamini. Baraza la wadhamini husajiliwa katika ofisi za Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA). Kwa hiyo mkishakamilisha kusajili dhehebu lenu katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani mnapaswa pia kuanza mchakato wa kusajili baraza la wadhamini wa dhehebu hilo. Utaratibu wa usajili wa baraza au muungano wa wadhamini nitauelezea katika kipengele kinachofuata.
Ni jambo la muhimu sana dhehebu, kanisa au huduma kuwa na mwanasheria wake ambaye atakuwa akishughulikia maswala yote ya kisheria ya dhehebu, kanisa au huduma hiyo. Mwanasheria huyu atawasaidia pia hata katika hatua za awali za usajili pamoja na maswala mengine muhimu ikiwemo uandaaji wa nyaraka muhimu.
Msifanye maamuzi yoyote yanayohusisha maslahi ya watu katika huduma au kanisa au mustakabali wa kanisa pasipo kumuhusisha au kuomba ushauri kwa mwanasheria. Matatizo mengi yametokea makanisani na misikitini kwa sababu tu, viongozi hawakuzingatia maswala muhimu ya kisheria ambayo wangeyapata kama wangekuwa wameshauriwa vyema na mwanasheria. Ni bora kuingia gharama, kuliko kuja kupata hasara ambayo hamtaweza kuilipa.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments