Maurice,
Unadanganyika tu, miradi ya utafuataji wa gesi na mafuta ni ya siku nyingi hapa nchini, haikuanza na Kikwete, yeye kadandia tu treni kwa mbele!
Suala la ahadi za Kikwete ni ulaghai mtupu; kawakaghai wahaya kuwajengea meli kubwa zaidi katika ziwa Victoria na hakuna kichofanyika mpaka hivi sasa zaidi ya meli iliyopo kuzimikia ziwani hivi majuzi na kusababisha taharuki kubwa kwa abiria waliokuwemo humo. Hilo la bandari ya Bwagamoyo likikamilika basi ujue ni kwa ajili ya kuendelea kuhamisha rasilimali zetu kwa kasi kubwa kwenda Uchina maana tayari jamaa wameshaanza kutufilisi! Hebu iangalie tu bandari ya Dar es salaam, imelisaidia vipi taifa hili chini ya utawala wa msanii huyu? Unaikumbuka kauli ya rais Kagame?
Kuhusu kutangatanga, hujui kuwa jamaa huenda kula maisha tu huko? Unaweza kuniambia katuletea mangapi zaidi ya kupoteza tu pesa zetu? Ziara hizo zingelikuwa na tija, hivi si kweli kuwa kwa hiyo idadi yake kubwa, si tungelikuwa tunaishi kwenye paradiso inayoitwa Tanzania? Je ulimuona wakati akibembea Cuba? Unakumbuka jinsi alivyokwepwa na mmoja wa marais wenyeji wake kule ughaibuni? The guy is a true shame to this country!
Hivi unajua ziara ya Obama ilikuwa na malengo gani? Imetusaidia nini sisi watanzania zaidi ya sifa tu za kijinga? Unakumbuka wakati Obama anazungumzia kufanya biashara na Tanzania, mshikaji wetu alikuwa anaona sasa kapata fursa pekee na adimu ya kuomba msaada? Naam kidume kigawa pesa kimejileta chenyewe mpaka chumbani mwako!
Kuhusu mchakato wa Katiba, Maurice, it was a terrible shame of the century; katiba hiyo mpaka marehemu kapiga kura! Kwanza mchakato wa katiba haukuwa kwenye ilani ya uchaguzi ya chama chake, alidandia tu hoja ya upinzani kwa lengo la kuivuruga! Wapinzani walipotoka nje, ama wangelisikilizwa hoja zao na kuzifanyia kazi stahiki, ama mchakato mzima ungelisitishwa maana ilikuwa ni hoja yao, na matokeo yake ni kuwa kilichopatikana ni kibaya kuliko kilichokuwepo ambacho kingeliweza kufanyiwa marekebisho tu kwenye tume ya uchaguzi na suala la wagombea binafsi. The rest vingelifanywa na wenye appetite ya kuipatia nchi hii katiba bora siku za usoni!
SA.
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAPPZ%3DWwBAOH8aFy8K_M%3DjwagwEZPNN91M9GnM3Jrh5MUmAgsWQ%40mail.gmail.com.
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAKWnvr_1tzcjUvZ0o3uZbLpeojAUx%2BFnM35-R57bB0u5Vn46Cg%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments