[Mabadiliko] LUDOVICK WA CHADEMA: SIMULIZI YANGU- Gazeti CHANGAMOTO

Tuesday, November 18, 2014

LUDOVICK WA CHADEMA;

SIMULIZI YANGU

     Kwa wafuatiliaji wa taarifa katika vyombo vya habari na hasa magazeti wanafahamu kuwa nimekuwa nikihusishwa na matukio kadhaa ya kisiasa na hatimaye pamoja na Lwakatare mkurungezi wa ulinzi wa CHADEMA Taifa, Tulifunguliwa mashitaka na kuwekwa gerezani ambapo mimi nilikaa kwa miezi mine Kabla ya kupata dhamana. Hakika yalisemwa mengi na bado yanaendelea kusemwa na labda masimulizi haya yataibua mambo mengine zaidi.

        Ingawa habari kuhusu mimi ziliandikwa sana mfululizo kwa zaidi ya miezi mitatu lakini tangu nipate dhamana mwaka mmoja na miezi miwili sasa bado naona jamii haijapata kujua kwa undani wala ukweli wa nini hasa kilitokea. nimeona kwa macho yangu mwenyewe namna ambavyo kuna uwezekano wa jamii kupotoshwa juu ya jambo Fulani na ikajikuta inaamini  tofauti na ukweli.

         Ninaandika simulizi hii ili kuelezea uhalisia wa kilichotokea na kile ninachoweza kukiita " simulizi yangu"(the side of my strory).

   Ni muhimu kuzingatia kuwa bado ninayokesi mahakamani. kwa hiyo simulizi hili halitahusu masuala ambayo yanaweza kuingilia mwenendo wa kesi na uhuru wa mahakama. Hayo tutayaongea baada ya kesi kumalizika. Inshallah!

         Kwa hiyo simulizi hili haina lengo la kujitetea  wala kutoa tuhuma kwa yeyote, bali jaribio la kuelezea kilichotokea lakini pia kusahihisha uongo na upotoshaji uliofanywa na watu mbalimbali juu ya matukio niliyohusishwa nayo.

       Na kwa ufupi tu nimezaliwa bukoba vijijini mwaka 1982, katika familia ya mwl.ludovick Paulo na Savera Telesphor, watoto Sita wote wa kiume, mimi nikiwa mzaliwa wa nne. Nimewahi kuishi Mwanza Morogoro, Songea Daresalaam na Mbeya. Nimeoa na nina mtoto mmoja.

        Nimesoma shule ya msingi na Kumaliza darasa la saba mwaka 1997 na kujiunga nyakato secondary iliyopo Bukoba kwa kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 2001. Mwaka 2002 nilijiunga na seminari katoliki ya mt. Francis De sales Morogoro ambapo nilimaliza kidato cha sita mwaka 2004. Baada ya hapo  nilijiunga na malenzi ya upadre katika shirika la mt. Vincent  wa  paulo  na kupokelewa hapo mwaka 2005. Kwa muda kabla ya kuingia shirika hilo, nilifundisha Rugambwa girls, high school – ya Bukoba.

 nilifanya mwaka wa malezi hadi sept,nilipoanza kusoma shahada ya falsafa katika chuo cha wasalvatori (salvatorian Institute of philosophy and theology)chuo hiki ni affiliate ya pontifical university Urbaniana  cha Roma Italia. katika mchakato huo nimewahi pia kukaa kwa muda kibosho  major Seminary Moshi kabla ya kuamua kuacha malezi ya upadre na mwaka 2008 nikajiunga na chuo kikuu kishiriki cha ualimu cha DUCE ,ambako niliondoka mwaka 2011.

Nilipangiwa kufundisha Singida lakini sikuendelea na kazi ya ualimu huko,badala yake nilijikita katika siasa na katika mitandao ya jamii nikiendesha Mjenjwa  blog. nitafafanua zaidi juu ya baadhi ya masuala haya huko mbele.

 

KUJIHUSISHA NA SIASA

Tangu kale nikiwa kidato cha pili mwaka 1999,nimekuwa mfuatiliaji mkubwa wa siasa nikisoma kila wiki magazeti ya RAI enzi hizo likiandika chambuzi mbalimbali.nilichaguliwa kiranja mkuu wa shule na nilikuwa na mahusiano na viongozi kadhaa wa CCM mkoa wa kagera siku hizo,Mzee Senguo,nadhani katibu wa CCM mkoa na ndugu kagashe. pia nilimfahamu kapteni mstaafu kateme diwani wa kata yangu CCM (baadaye mwenyekiti wa halmashauri ya BKB vijijini)

Lakini baada ya kuingia seminari,nilikuwa nimebadilika sana interest kwenye siasa na hapo nilifikiria zaidi malezi ya upadre na mafunzo hayo na kwa kweli hakuna ruhusa kujihusisha na siasa katika seminari

   Nakumbuka nilikuwa  nikipenda sana makala za padre privatus Karugedo. Nilipata shida kwa sababu Karugendo alikuwa hatazamwi vema  na walezi wangu na kushabikia  makala zake ilitafsiriwa kama kukubaliana na  mitazamo yake hasi  juu ya baadhi ya mafundisho ya kanisa katoliki.

          Mwaka 2006, nikiwa nasoma Falsafa, nilifahamu juu ya chama cha chadema kuzaliwa upya. Hapo nikasikia kuwa kina "Falsafa" ya Nguvu ya umma. Nilipenda sna sana kujua msingi wa falsafa hiyo kwa hiyo nilipopata likizo, nikiwa Dar-es-ssalaam,nilitafuata ofisi za chadema  na hapo nilikutana mara nyingi sana na John Mnyika – wakati ule akiwa anaonekana hata kwa macho kuifuata na kuiamini falsafa ya chama.

      Tulikaa  na mnyika kwa masaa mengi karibia kila siku nilipokuwa Dar-es-salaam tukijadili mambo mbalimbali , nikimsaidia kuelewa baadhi ya maswala ya kikanisa  yaliyokuwa yanamtatiza. Tulikuwa tunakutana na Akani David Kafulila wakiwa wadogo kwelikweli. nakumbuka siku nyingine Mnyika hakuwa na hela ya chakula cha mchana na mimi nilimnunulia lunch.

Lakini hata wakati huo hatukuruhusiwa kufanya siasa seminari  na hakika hilo halikuwa suala la kipaumbe.,hata hivyo mapenzi yangu kwa chadema yaliendelea na nilipoacha  malezi ya upandre na kuanza chuo kikuu pale DUCE, mwaka 2009 nilijiunga na kukabidhiwa rasmi kadi ya chadema na Erasto Tumbo akiwa Afisa wa habari na uenezi na nilikabidhiwa  kadi hiyo makao makuu ya chama .baadaye nilikuwa mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA chuo cha DUCE…itaendelea wiki ijayo…

0752 814961

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CACMr6Qg-5zaw6udtCDz0AtKof1sgw1%3Di0vfU0d72AE%3DWbTeb0A%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments