[Mabadiliko] ACT: Mwigamba atimuliwa ukatibu mkuu - MTANZANIA

Wednesday, November 12, 2014

Naileta kama nilivyoikuta JF, labda msemaji mkuu wa ACT hapa jamvini anaweza kutujuza. Au ni ni ukanjanja wa MTANZANIA


Katibu Mkuu wa ACT- Tanzania Samson Mwigamba amesimamishwa uongozi ndani ya chama hicho kwa tuhuma za ukiukwaji wa maadili,kuvunja katiba na ubadhirifu ndani ya chama hicho.

Taarifa kutoka kwa waasisi wa chama hicho ambao ni Greyson Nyakarungu na Leopold Mahona zinasema mbali na Mwigamba pia chama hicho kimetoa karipio kali kwa viongozi waandamizi wa chama hicho Professor Kitila Mkumbo na Habib Mchange kwa tuhuma mbalimbali.

Ikumbukwe Samson Mwigamba,Prof Kitila Mkumbo na Zitto Kabwe walitimuliwa uongozi ndani ya CHADEMA mapema mwaka huu kwa tuhuma kama hizi na kusababisha kukimbilia chama cha ACT Tanzania.

Source:Mtanzania Jumatano

Updates zaidi....

Waasisi wa ACT Tanzania Greyson Nyakarungu na Leopold Mahona waliwaambia waandishi wa habari jana kuwa waliwakaribisha Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba ndani ya chama hicho kwa nia njema kumbe ni wasaliti na walaghai wakubwa.

Alisema kwanza kina Mwigamba wanajivika uasisi wa ACT huku wakijua si kweli. Pia kina Mwigamba wanatuhumiwa kwenda ofisi ya Msajili kubadili nembo ya chama kinyume cha utaratibu. Pia wanatuhumiwa kusajili katiba nyingine kinyume na Katiba waliyoandaa waasisi na kupatia chama usajili.

Nyakarungu amesema tayari Waasisi halali wa ACT wameshamwandikia barua msajili wa vyama kumuelezea juu ya uasi unaofanywa na kina Mwigamba na Kitila.


--
Awesome.
''Everybody is a genius. But if you judge a fish by its ability to climb a tree, it will live its whole life believing that it is stupid." 

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAJJMsUvxDQqLSXXvjtodmT-vi4sE2FgwEAK3%3DyHYihrCcEvJeQ%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments