[wanabidii] Wachagga na 'sale' linavyotumiwa kuficha maovu na kupalilia unyanyasaji

Tuesday, October 07, 2014
Imeelezwa kuwa vitendo vya ukatili wa kijinisa vitaendelea iwapo jamii haitaacha kukumbatia tamaduni potofu kama vile watu kuombana wapatane au 'mambo yaishe' kwa kutumia jani maarufu kwa kabila la Wachaggga mkoani Kilimanjaro lijulikanalo kwa jina la 'sale'.

Wananchi, Wanasheria, Dawati la Jinsia na Watoto wakitoa maoni yao kuhusu mila hiyo wamesema kutumia 'sale' kutaendeleza ukatili wa kijinsia miongoni mwa jamii.

Mwananchi mmoja amesema kwa mfano, katika Kata ya Uru Shimbwe katika vitongoji vya Temboni na Shimbwe kuna baba mmoja mnywaji wa pombe haramu ya gongo alimbaka mtoto wa miaka 6 na hakuna kesi iliyofunguliwa baada ya wahusika 'kuyamaliza' kwa 
kutumia 'sale.' Pia katika shule ya Sekondari Shimbwe, wanafunzi wawili walipata mimba lakini hakuna kesi iliyofunguliwa. Ulinzi wa watoto katika Kata hiyo umetajwa kuwa mgumu hasa kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Baadhi ya Wanasheria walioko katika mazoezi wamesema mtu yeyote anayefanyiwa ukatili wa kijinsia anapaswa kuripoti polisi na si vinginevyo.

Kaimu Afisa Ustawi wa Jamii, Agness Urasa amesema mila ya 'sale' ni potofu na ingawa katika ofisi hiyo, zipo ofisi zinazohusiana na masuala ya unyumba wahusika husuluhishwa na ukoo ama mdhamini wa ndoa na inaposhindikana, ofisi yao huchukua hatua zaidi za usuluhishi.

Taarifa ya Josephine Sanga, Sauti ya Injili, Moshi.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments