[wanabidii] UKWELI KUHUSU AG WA ZANZIBAR KUAMBATANA NA ULINZI KATIKA MAENEO YA BUNGE MAALUM.

Thursday, October 02, 2014
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE MAALUM

Simu:  +255 026 2322696
Fax No. +255 026 2323116
Barua pepe: info@bungemaalum.go.tz

Ofisi ya Bunge Maalum,
S.L.P. 901,
DODOMA.

14 Julai, 2014

UKWELI KUHUSU AG WA ZANZIBAR MHE. OTHMAN MASOUD OTHMAN  KUAMBATANA NA ULINZI KATIKA MAENEO YA BUNGE MAALUM.


Kumekuwa na Taarifa potofu zinazosambazwa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii ya kuwa "Mwanasheria Mkuu Zanzibar Othman Masoud Othman amekamatwa baada ya kupiga kura ya hapana Bungeni leo"

Tunapenda kuutarifu Umma wa Watanzania kuwa, taarifa hizo sio sahihi na ni porojo zenye kutaka kuleta hisia potofu kwa wananchi kuhusu kiongozi huyo.

Ukweli wa Jambo hili ni  kuwa Mhe. Othman Masoud Othman ametekeleza haki yake ya 
Kidemokrasia  ya kupigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekeza katika Bunge Maalum leo.  Ambapo katika kura alizopiga, ameweza kuzikubali baadhi Ibara na kuzikataa ibara nyingine katika rasimu ya Katiba inayopendekezwa.

Pengine hatua hiyo ya kuzikataa baadhi ya Ibara, haikuwafurahisha baadhi ya Wajumbe na hivyo kuleta majibishano ndani ya Bunge Maalum wakilalamikia uamuzi wake huo.

Kutokana na hofu hiyo ya baadhi ya Wajumbe kuanza kupinga uamuzi wake huo ndani ya Bunge, Ofisi ya Bunge Maalum kama ilivyokawaida kwa kila mjumbe, imeweza kumpatia Ulinzi Maalum wakati akitoka Bungeni hadi alipoondoka katika viwanja vya Bunge ili asiweze kubugudhiwa kwa namna yoyote ile kutokana na  uamuzi wake huo.

Suala hili limechukuliwa kipropaganda na kuanza kueneza uongo katika mitandao ya kijamii kuwa Mhe. Othman amekamatwa baada ya kupiga kura ya hapana.

Tunapenda kuwahakikishia Watanzania wote kuwa Mhe. Othman hajakamatwa bali alipewa ulinzi katika Maeneo ya Bunge Maalum jambo ambalo hufanyika kwa kila mjumbe ambaye kwa namna moja ama nyingine itaonekana kuna dalili za kubugudhiwa katika Maeneo ya Bunge kutokana na uamuzi au kitendo alichofanya. Na kutokana na hali ilivyo, ulinzi wake umeimarishwa pia mahali alipo kwa hivi sasa mpaka atakapomaliza kazi yake hapa Dodoma.

Kanuni za Bunge Maalum zimempa madaraka Katibu wa Bunge Maalum kusimamia masuala yote ya Ulinzi na Usalama kwa Wajumbe na Maeneo yote ya Bunge Maalum.

Imetolewa na Idara ya Habari
Ofisi ya Bunge Maalum
Dodoma
1 Oktoba, 2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments