WanaCCM,
-- Mkutano Mkuu wa uchaguzi uliotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 11/10/2-14 umeahirishwa.
Viongozi katika kamati ya Halmashauri Kuu ni 5 na kati ya hao 3 wamepitisha na kukubali kuahirishwa kwa uchaguzi na 2 bado hawajajibu.
Sababu:
- Wengi wa wanachama siyo hai kwani ada za wanachama hazijalipwa.
- Wapiga kura wengi hawana kadi.
- Kila muombaji uanachama ni lazima kamati iliyopo ipitishe ombi lake.
- Hadi asa haijajulikana tuna wanachama wangapi na hatuwezi kuweka chama hatarini.
- Kila mwanachama anayo haki ya kugombea, mgombea wa nafasi hawezi kujitangaza kabla ya Kamati Kuu haijaidhinisha na kueleza wanachama.
- Katiba izingatiwe kwa nguvu zote kuhakikisha wanachama wakereketwa na wagombea wenye maadili yanayokubalika na jamii wamepta nafasi za kugombea.
- Kamati Kuu ya uchaguzi ndiyo iwe na mamlaka ya kuidhinisha majina ya wagombea na kutangawa na Mwenyekiti wa kamati hiyo kwa idhini ya Mwenyekiwia wa CCM.
- Mwenyekiti wa CCM ndiye anayo mamlaka ya kuongoza vikao vyote vya kujadili na kuidhinisha wagombea baada ya uchunguzi wa maadili ya mgombea ndani ya Kamati ya Uchaguzi.
Hofu ya viongozi waliokubali kuahirishwa ni hizi zifuatazo:
a) Usajili holela wa wanachama unaweza kuweka maisha ya chama chetu hatarini kwa kuingiliwa na mamluki
b) Kuchambua maadili ya wagombea nafasi ndani ya chama ili tusihatarishe usalama wa chama.
c) Katiba kutupiliwa na kufanya maamuzi ya binafsi kwa faida binafsi za wagombea.
Kwa hayo machache, wengi wameamua kusitisha uchaguzi wa viongozi wa CCM - New York na vitongoji vyake.
Viongozi wa Kamati Kuu ya CCM New York ni hawa wafuatao:
Mwenyekiti: Masudi H. Maftah
Katibu: Akina Seif
Katibu Mwenezi: Peter Kiula, Isaac Kibodya na Professor Lwiza Kamazima.
Naomba WanaCCM wote wa New York na vitongoji vyake wavumilie hali iliyopo sasa hivi na Mkutano wa Viongozi utafuatiwa na Mkutano wa Wanachama ili kujadili mustakabali wa Chama na uchaguzi wa viongozi.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
UONGOZI CCM/ NEW YORK
MWENYEKITI
MASUDI H. MAFTAH
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments