Majibu yangu kama Muislamu kwa VIHOJA pinzani dhidi ya kuwapo kwa Mahakama ya KADHI.
Naaam!!! Nimejiridhisha pasi nashaka kuwa wameshindwa kujenga HOJA kuonyesha madhara ya uwapo wa Mahakama hiyo nchini Tanzania licha ya kutumia gharama kubwa kuipinga.
Wakati mwingine nastuka sana unamkuta Kiongozi mkubwa na mwenye dhamana kubwa pengine mwenye Elimu nzuri(MASTERS) anasimama na kusema Mahakama ya Kadhi italeta BOKO HARAAM.
Maswali mepesi kwa Viongozi hawa:-
1- Hivi ni kweli BOKO HARAAM wanagombana kisa uwepo wa Mahakama ya Kadhi nchini mwao......?
2-Hivi nchi kama Kenya , Rwanda, Uganda Malawi ,Afrika Kusini wana Mahakama ya Kadhi kwenye Katiba zao kwanini huko hakuna BOKO HARAAM......?
3- Hivi ni kweli viongozi wetu wameshindwa kujua kuwa Mahakama ya Kadhi ni IBADA kwa waumini wa Kiislamu na itajishughulisha na mambo machache sana kama Talaka. Ndoa, na Mirathi.......?
4- Joseph KONNY anapigana UGANDA akitaka nchi yake iongozwe kwa Amri "10" za MUNGU, Je Konny nae ni zao la Mahakama ya Kadhi au uwepo wa BALOZI mbili zikiwakilisha nchi moja yaani ("VATICAN" na "ITALY")......?
5- Kweli viongozi hawa hawajui kuwa wamekuwa wakishughulikia mambo haya ya Waislamu kama Talaka, Mirathi, na Ndoa katika Mahakama za Kawaida bila kuwa na ujuzi wa Kiislamu.......?
DHANA IMEJENGEKA KUWA KILA JAMBO BAYA NI LA MUISLAMU.
Kwa bahati mbaya DHANA hii imejengwa na serikali ya CCM na watu wanaishi nayo, Huku serikali ikichekelea kufanikiwa kumfanya muislamu kama Raia daraja la mwisho.
Kelele zilipigwa na Waislamu kuhusu mgawanyo wa vyeo vya kuteuliwa viwe kwa usawa, Majibu yalikuwa ya KIJINGA eti.. Ninyi waislamu hamkusoma ha ha ha ha ha !! Hivi kama ukitambua tu waislamu nchi wapo 10m huwezi kupata waislamu waliosoma 200 tu kutoka hao 10m na Baraza lako la mawaziri likiwa na watu 60 unashindwaje kupata 30 miongoni mwa hao 200 kama kweli nchi hii waislamu thamani yao ni kama Wakristo......?
Hali hii ya mgawanyo wa hovyo wa madaraka kwa vyeo tu vya KUTEULIWA kukiwa hivi hebu jisumbue kama mimi utazame Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala ,Wilaya, Wakurugenzi, Makabu wa Wizara Mawaziri na Manaibu Mawaziri, Jumla ya watendaji hawa wote hawafiki 500 je tunashindwa kuwa gawa kwa usawa tukizingatia waislamu wawe 10m tena na kutokusoma kwao wanakosekama waislamu 500 ili usawa upatikane....?
Pale Bungeni katika bunge la JMT karibu idara zote hadi Katibu wa Bunge Thomas Kashilila ni Wakristo kasoro Idara ya wale wanaobeba "SIWA" ndio inaongozwa na muislamu, Je nao walikosa kuweka usawa kwakua hakuna muslamu aliyesoma....?
HAYA HAYAKUJA KWA BAHATI MBAYA NI MPANGO UNAOSIMAMIWA NA CCM
Tunako elekea waislamu wataukana uislamu wao ili wafaidi matunda ya kuwa waumini wa dini pendwa na serikali ya CCM.
Au wataukana Uislamu wao ili kukwepa kuwa shabaha ya misukosuko na mateso nchi kwakua kila jambo baya serikali ya CCM wanalihusisha na Waislamu,
Utafuti unaonyesha kuwa wajumbe wa nyumba kumi kumi wa ccm 80% ni waislamu kwahiyo hivyo ndio vyeo walivyotugawiya CCM ili kuimalisha chama kwajili ya kutengeneza MFUMO KRISTO juu.
UDANGAYIFU NA UONGO WA SERIKALI YA CCM KWA WAISLAMU.
Waziri mkuu Mhe Pinda aliwambia waislamu wasubiri mahakama ya Kadhi mswada utapelekwa bungeni mwezi wa kwanza mwakani sasa hebu wewe muislamu tafakari uone ulivyodanganywa.
1-Tunaunda Katiba mpya ili hii iliyopo tuachane nayo nayeye mhe Pinda anasema tusiweke huku hiyo mahakama ya Kadhi bali tukaiweke kule ili Katiba ile ikikoma kutumika na mahakama ya Kadhi ikome kule kule je hujadanganywa....?
2-CCM waliweka mahakama ya Kadhi kwenye ILANI yao mpaka sasa hawajatekeleza leo watatekeleza kwa ahadi hewa na kwanini ikawekwe kwenye katiba inayokufa isiwekwe kwenye hii mpya....?
KURA YA HAPANI NI IBADA KWA MUISLAM
Naaam nimetimiza wajibu wangu kwajili ya kusaka pepo ya mungu-Ishallah!
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments