[wanabidii] JAJI JOSEPH WARIOBA AANZISHA KAMPENI ZA KULIGAWA TAIFA

Thursday, October 16, 2014
Taarifa inaripotiwa kutoka mikutano inayofanywa na Jaji Joseph Warioba inaeleza kuwa Mzee huyu ameanzisha kampeni yenye siasa chafu.
Tofauti na hadhi aliyonayo ya Waziri Mkuu Mstaafu,Makamu wa Rais Mstaafu,Jaji Mstaafu na kiongozi wandamizi enzi za Nyerere na Mzee Mwinyi, Warioba ameanzisha uchonganishi Kati ya serikali na wananchi, ameanza kupandikiza chuki Kati ya Watanzania wa bara na Zanzibar, 

Mzee Warioba ameanzisha kampeni hiyo akishirikiana na viongozi wa Ukawa, huku ziara zake zikichangiwa mamilioni ya shilingi ili kukamilisha mpango huo.

Katika vikao anavyovisimamia yenye mwenyewe agenda kuu ni

1. Wananchi wasiunge mkono kauli ya Rais aliyotoa Juzi kwenye kilele cha mbio za mwenge Tabora, kuwa Vijana wasikubali ulaghai huo kwani maslahi yao hayamo kwenye katiba inayopendekezwa.

2. Wananchi wahamasishwe kupiga kura ya HAPANA.

3. Mchakato wa katiba urudiwe ili zipatikane serikali Tatu maana muda ndio huu, hatuhitaji muda mwingine.

4. Kura ya maoni isipigwe Sasa ili Wananchi wajue walivyosalitiwa na CCM.

5. Watanganyika wananyonywa na Wanzanzibari kwenye keki ya Taifa.

Mzee Warioba amepangiwa kutembelea Mikoa ya Arusha,Kigoma,Kilimanjaro,Mbey a,Mwanza,Dar es Salaam,Tabora,Mtwara na Mara.

Ili kuanza ziara hiyo iliyochangiwa na UKAWA Mzee Warioba hakwenda Tabora, Alienda Butiama akiambatana na Mjumbe Mwingine Joseph Butiku, Wakiwa hapo Butiama walifanya kongamano na Wazee, lakini kazi hiyo iliingia dosari Wakiwa katikati ya shughuli hiyo baada ya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Butiama kuhoji kwanini wanahubiri habari ya serikali tatu wakati Mwalimu aliamini Katika serikali Mbili? Baadhi ya Wazee walianza kuzomea na wengine kuondoka na kongamano likaisha kwa kunusuliwa na Ndugu wa Mwalimu Nyerere.

Siku ya Jana Warioba alikuwa Nyamuswa Bunda, hapo alikusanya ya makundi ya Vijana na Wazee, kazi hiyo imeratibiwa na UKAWA ambao walipanga kumpokea eneo la Lamadi Mpakani mwa Simiyu na Mara,kazi hiyo ilishindikana baada ya pesa kuchelewa kutumwa. Wakaahidi kumsindikiza akimaliza ziara yake Mkoa wa Mara.

Viongozi wa CCM wilaya ya Bunda walihoji kwanini hawakuhusishwa kwenye ziara hizo ambao mara nyingi humpokea walijibiwa kuwa hawahitajiki.
Kikao cha Vijana na Wazee wa Eneo la Ikizu kilijumuisha Baadhi ya viongozi wa CCM ngazi ya kata,kitendo hicho kiliwaudhi viongozi wa chadema, kwenye mikutano yote miwili Jaji Warioba alisisitiza agenda tajwa hapo juu huku akisisitiza viongozi hao kuipinga katiba, lakini baada ya Kikao hicho Baadhi viongozi na Wazee walibeza ujumbe huo kuzusha ubishani.

Katika Vikao hivyo Mzee Warioba aliwachinjia ng'ombe na kuwaandalia chakula Kama sehemu ya ushawishi.

Leo tarehe 16/10/2014 atakuwa na kongamano la kuendeleza ajenda hizo chafu katika Ukumbi wa Herieti Bunda Mjini, gharama za Ukumbi huo zimechangwa Jana Katika maazimio ya vikao vya chadema.Tutawajuza yote yatakayojadiliwa leo.

Huyu ndiye Warioba anaeneza siasa chafu na uchonganishi wa Wananchi na serikali huku akisambaza sumu ya kuwatenga Wazanzibari.

Source: Mjumbe Katika ziara na mipango ya Warioba na Ukawa.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments