VUGU VUGU LA UKAWA KUELEKEA IKULU 2015
Mambo mawili ni dhahiri katika medani za kisiasa nchini mwetu hivi sasa;
Mosi, imeshakuwa bayana kwamba wanasiasa wamekwishakubaliana kwamba Katiba Mpya ipatikane baada ya uchaguzi wa mwaka 2015. Wanachobishania hivi sasa ni namna tu ya kuusitisha mchakato huo wa uandikaji wa Katiba.
Pili, ni ukweli usio shaka kwamba vuguvugu la UKAWA limevuka malengo yake ya awali ya kuwa Umoja wa Katiba na sasa linataka kutumika kama karata muhimu kuelekea 2015.
Kwa bahati mbaya, mpaka sasa sijabahatika kusoma uchambuzi wa kina na usio wa kishabiki kuhusu jinsi vuguvugu la UKAWA linavyoweza ( au kushindwa) kuubadili mwelekeo wa siasa zetu kuelekea Uchaguzi Mkuu hapo mwakani.
Ninatoa rai kwa masogora* wetu kwenye medani za siasa watufanyie uchambuzi wa nafasi ya UKAWA ambao utakuwa ni wa kina na utaoyadadavua mambo paruwanja* pasi na ukereketwa!
Profesa Kitila Mkumbo! Kwanza hongera kwa Uprofesa Mzee! Tunataka uchambuzi Prof! Bila shaka ule uchambuzi wako wa awali wakati wa chaguzi ndogo za udiwani na ubunge kwamba ''CCM is stabilising, CHADEMA is shrinking and CUF is disappearing'', yaani ''CCM inaimarika, CHADEMA inasinyaa na CUF inatoweka ( Kwenye siasa za Bara )'' itabidi uuchunguze tena! Au waonaje?https://groups.google.com/forum/#!topic/wanabidii/Vo5DAAxezX8
Mzee wetu Dk Azaveli Lwaitama, uko wapi uchambuzi Mzee? Bila shaka utakwenda mbali ya kile ulichokisema Mlimani City kwenye Mkutano Mkuu wa CHADEMA kwamba iwe isiwe UKAWA wakisimamisha mgombea mmoja 2015 lazima CCM ing'atuke madarakani hata wakichakachua vipi!
Ndugu Chambi Chachage ( Udadisi Mdadisi) nimesoma uchambuzi wako wa hivi karibuni kuhusu mchakato wetu wa Katiba baada ya UKAWA kukutana na JK. Kazi nzuri sana! It is such a brilliant piece. Andikia na hili Mzee ( Ah sorry! Ni kijana) http://udadisi.blogspot.com/2014/09/katiba-mpya-ukikimbia-nchale-ukisimama.html
Jenerali Ulimwengu upo Mzee?
Haya na wachambuzi wetu magazetini na mitandaoni tuelezeni, mwalionaje vuguvugu la UKAWA kuelekea 2015?
-- Mambo mawili ni dhahiri katika medani za kisiasa nchini mwetu hivi sasa;

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments