Lakini hata wangekuwepo wanaoamini hivyo lakini ukweli haukwepeki kuwa rais wa Tanzania anaweza kutoka chama chochote ikiwa ni pamoja na kutoka nje ya CCM, nah ii inawezekana sana leo kuliko ilivyokuwa jana.
Ni kutokana na ukweli huo mimi napendekeza kujadili nafasi ya UKAWA katika kutupatia rais.
Kwa mujibu wa Katiba tuliyonayo na ambayo inaelekea huenda ndiyo ikatumika uchaguzi ujao, UKAWA kama UKAWA haina uwezo kikatiba kujitokeza kuomba uongozi. Hii imewezekana Kenya na ni kwa sababu ya Katiba yao. UKAWA haiwezekani maana haijaandikishwa na wakijaribu kuiandikisha sasa maana yake waue vyama vyao na wakijaribu hilo huenda na UKAWA ikayeyukia huko.
Pamoja na hayo UKAWA inaweza kutupatria rais. Si inaweza tu bali rais huyo anaweza kuja kutatua matatizo tunayokabiliana nayo kama taifa.
UKAWA inaundwa na vyama vikuu vitatu yaani CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi.
Ukiisoma sawasawa utaona kwa mujibu wa jina lake inakwisha mara baada ya mkakati wa kulipatia taifa hili Katiba yake ukikamilisha lengo.
Lakini pamoja na hayo ni dhahiri kuwa UKAWA imewaogeza wapinzani karibu kuliko wakati wowote ule katika historia ya vyama vingi. Huku nyuma vyama yetu hivi viliwahi kujaribu umoja vikashindwa. Kwa mawazo yangu zamu hii vinaelekea kufanikiwa kuunda umoja utakaodumu kwa sababu aliyekuwa anavivuruga vyama hivi kimoja kimoja na katika kuunda umoja ni mmoja na simtaji lakini kwa sasa vyama vyenyewe vimemjulia nam pia kaishiwa mbinu.
Jambo la pili ni kuwa vyama hivi ukizisoma sera zao zinaelekeana kwa namna kubwa isiyo wazi. Kwa hiyomlicha ya kuungana kwa sababu ya kuitafuta katiba ni rahisi kuundana kwa sababu ya sera na namna ya utekelezaji wa sera hizo. Sijui kama nitatibua nikisema sera zao zinafanana kwa sababu matatizo wanayokabiliana nayo yanafanana. Kuukomesha ubadhilifu, na kutumia raslimali kuendeleza nchi na wananchi. Mambo haya mawili yanatosha kuwaunganisha na kuondoa tofauti za mambo ya undani wa sera za kila chama.
Ili UKAWA waweze kuunda serikali ni lazima wakubaliane mambo Fulani ya msingi:
Kuweka resa pamoja na kuwa na sera zinazo fanana na wote wakazisemea hizo.
Kukubali kumuunga mkono mghombea mmoja wa urais kutoka chama chochote bila kujali nguvu ya chama hicho. Mfano CHADEMA ina nguvu sana kuliko vingine. Kama Mgombea wao atatoka CUF kuwa tayari kumuunga mkono kwa nguvu zote.
Vyama hivyo kuwa tayari kumuachia rais huyo kuchagua mawaziri kuroka popote kama anavyoona na isitokee chama Fulani kusema kinaondoa wanachama wake katika serikali bila kutumia utaratibu maalum.
Mgombea urais kuwa tayari kuunda serikali ya mseto. Achague mawaziri wanaofaa bila kujali wanatoka chama gani na hao mawaziri wakiwa kwenye kazi zao wasiutumie uchama kuweka misimamo ndani ya serikali
Nafasi za wabunge nazo zinahitaji 'kujikana'. Tume ya UKAWA ya kuchambua majina ya wagombea iwe huru, makini na adilifu kiasi itamchambua mgombea kwa kumuangalia yeye uwezo wake na kukubalika kwake katika jamii bila kujali anatoka chama gani. Yaani kati ya wagombea ote kama CHADEMA itatoa 50% CUF 30% na NCCR-Mageui 20% kwa sababu ya uchambuzi wa tume ya UKAWA vyama vyote view tayari kukubali na wala CHADEMA isitumie wingi wake kuwanyanyasa wengine na pia CHADEMA isitegemee kuwa 'kwa hiyo itatoa mawaziri wengi'.
Wakati wa Kampeni Mgombea atanadiwa na vyama vyote kwa pamoja. Hii itaangaliwa kwa makini wakati huo maana ndiyo itakayotoa mwelekeo wa uhai wa serikali yao. Sina mashaka na CHADEMA kwa kuwa na mfumo wa kujikinga na adui ambaye huenda mbinu mpya zitakuwa chache.
Wakifanya hayo yote na mengine wataweza:
Kukubaliwa na wananchi. Na wakichaguliwa wataweza kuliongoza taifa hili. Kama Kenya waliweza na Tanzania inawezekana.
Mru akiniambia nibashiri na mwanachama gani wa vyama hivi anaweza kuteuliwa kugombea na akaweza kuwaunganisha wanavyama hawa na watanzania nitatoa majibu mawili
1) UKAWA inao wanachama wa namna hiyo wengi. Na la pili ni.
2) James Mbatia wa NCCR Mageuzi.
Wengine mnasemaje kuhusu hilo?
Elisa Muhingo
0787 186 507
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments