Tanzania ni moja ya nchi ambazo watu wengi sana wanaamini katika uchawi. Watu wengi wanaamini katika imani za kishirikina ili kuweza kupata mafanikio kwenye kazi, biashara na hata maisha kwa ujumla. Zaidi ya asilimia tisini ya Watanzania wanaamini katika imani za kishirikina. Yaani kuna wale ambao wanazitumia kufanikisha mambo yao na kuna wengi ambao hawazitumii ila wanaamini kuna wanaozitumia kufanikisha mambo yao.
Hakuna haja ya kudhibitisha sana hili kwa sababu tumeshuhudiia mauaji ya vikongwe, na pia tumeshuhudia sana mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi au albino. Tumekuwa kila siku tukiona watu wanahubiri kuhusu Freemason na habari nyingine za kichawi na pia tumeona watu wakishuhudia kwamba walikuwa wanafanya mambo haya ya kichawi na hivyo kuua watu au kufanya mambo mengine ya hatari ili kufikia mafanikio.
Pamoja na matukio haya kumekuwa na hadithi nyingi sana huku mitaani kwamba baadhi ya watu waliofanikiwa au maarufu ni kwa sababu wametumia uchawi. Tumekuwa tukisikia kwamba wasanii maarufu na hata matajiri wakubwa wanawezeshwa na waganga au wamejiunga na Freemason. Hapa
Freemason ikichukuliwa kama kikundi cha watu ambao wanajihusisha na imani za kishirikina.
Swali ni je mambo yote haya yana ukweli? Imani hizi ni za kweli? Je uchawi unaweza kuleta mafanikio? Je ni kweli watu wanafikia mafanikio makubwa kupitia imani hizi za kishirikina?
Jibu ni hapana, uchawi hauwezi kumletea mtu yeyote mafanikio, bali mtu mwenyewe ndio anaweza kujiletea mafanikio. Nafasi ya uchawi katika mafanikio ya mtu ni kumpa imani isiyotetereka kwamba anaweza kufanikiwa. Kwa imani hii mtu anafanya kila anachoweza ili afikie mafanikio makubwa ambayo amehakikishiwa kwamba kupitia uchawi anaweza.
Hii inafanyaje kazi kwa binadamu?
Akili ya kila binadamu inaweza kugawanywa kwenye sehemu tatu, kuna akili inayofikiri na kufanya maamuzi (conscious mind), kuna akili inayopokea na kutoa kila unachofikiri ila haifanyi maamuzi (subconscious mind), na kuna akili yenye kuongozwa kwa imani (super-conscious mind).
Katika mafanikio na hata imani nyingine sehemu kubwa inayoathiri maisha yetu ni subconscious. Akili hii haiwezi kutofautisha kati ya mema na mabaya, yenyewe inapokea kila kitu kinachoingizwa (kwa mfumo wa mawazo) na kutoa vitu hivyo katika maisha ya kawaida. Ndio maana mtu anayefikiria kuumwa kila mara hupata ugonjwa kweli. Mtu anayezungumzia ajali kila mara huishia kupata ajali. Na mtu anayefikiria mafanikio kila mara huishia kupata mafanikio. Hii ni kwa sababu akili hii huvuta yale ambayo unayafikiri kila mara na kuyaleta kwenye maisha yako.
Kama ni kufikiria tu mazuri kwa nini kila mtu hafanikiwi?
Kama tulivyoona ni kwamba akili hii inapokea chochote kinachowekwa, haiwezi kutofautisha mema au mabaya. Mawazo yakishaingia yenyewe inayafanyia kazi na kukuletea yale mazingira. Sasa inawezekana umeshawahi kufikiria sana kuhusu kufanikiwa na akili yako ikaanza kukutengenezea mazingira hayo, baadae ukaingiza tena mawazo ya kushindwa, au wasiwasi hivi nitaweza kweli, au kusikiliza wanaokukatisha tamaa kwamba huwezi. Akili yako inachukua mawazo haya pia na kuandaa tena mazingira ya kushindwa. Hivyo unajikuta huwezi kufikia mafanikio kwa sababu huna uhakika na kitu kimoja unachokitaka.
Nini kinatokea kwenye uchawi au imani nyingine?
Kwenye uchawi au imani nyingine kinachotokea ni kwamba mtu anaaminishwa kwamba kwa kitu fulani atakachofanyiwa ni lazima atapata mafanikio makubwa. Kwa mfano mtu anaambiwa ukiwa na hirizi hii utapata chochote unachotaka. Mtu huyu anatembea na hirizi yake akiwa na uhakika asilimia mia moja kwamba atafikia mafanikio anayotaka, na kweli inatokea hivyo. Kilichompa mafanikio sio hirizi ila ile imani yake na mawazo kwamba lazima atafanikiwa kitu ambacho angeweza kukifanya hata bila ya hirizi.
Kwa wale wafuasi wa dini kuna miujiza mingi sana inatokea kwenye dini na imewahi kutokea. Miujiza yote hii inatokana na imani za watu kwamba wanaweza kupona, wanaweza kufikia mambo makubwa.
Hapa nimegusia machache sana na kwa juu ili upate picha ya jinsi gani mambo haya yanakwenda, unaweza kuendelea kujifunza zaidi ili kupata elimu ya ndani sana. Lakini ukweli ndio huu tuliozungumzia hapa.
Wiki ijayo tutaona ni jinsi gani masharti wanayopewa watu kwa waganga yanaweza kuwasaidia kufikia mafanikio makubwa wakati waganga wenyewe wana maisha magumu.
Nakutakia kila la kheri katika safari ya kufikia mafanikio makubwa, usidanganywe kwamba uchawi ndio maajabu ya wewe kufanikiwa, maajabu unayo mwenyewe kwenye kichwa chako.
-- Hakuna haja ya kudhibitisha sana hili kwa sababu tumeshuhudiia mauaji ya vikongwe, na pia tumeshuhudia sana mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi au albino. Tumekuwa kila siku tukiona watu wanahubiri kuhusu Freemason na habari nyingine za kichawi na pia tumeona watu wakishuhudia kwamba walikuwa wanafanya mambo haya ya kichawi na hivyo kuua watu au kufanya mambo mengine ya hatari ili kufikia mafanikio.
Pamoja na matukio haya kumekuwa na hadithi nyingi sana huku mitaani kwamba baadhi ya watu waliofanikiwa au maarufu ni kwa sababu wametumia uchawi. Tumekuwa tukisikia kwamba wasanii maarufu na hata matajiri wakubwa wanawezeshwa na waganga au wamejiunga na Freemason. Hapa
Freemason ikichukuliwa kama kikundi cha watu ambao wanajihusisha na imani za kishirikina.
Swali ni je mambo yote haya yana ukweli? Imani hizi ni za kweli? Je uchawi unaweza kuleta mafanikio? Je ni kweli watu wanafikia mafanikio makubwa kupitia imani hizi za kishirikina?
Jibu ni hapana, uchawi hauwezi kumletea mtu yeyote mafanikio, bali mtu mwenyewe ndio anaweza kujiletea mafanikio. Nafasi ya uchawi katika mafanikio ya mtu ni kumpa imani isiyotetereka kwamba anaweza kufanikiwa. Kwa imani hii mtu anafanya kila anachoweza ili afikie mafanikio makubwa ambayo amehakikishiwa kwamba kupitia uchawi anaweza.
Hii inafanyaje kazi kwa binadamu?
Akili ya kila binadamu inaweza kugawanywa kwenye sehemu tatu, kuna akili inayofikiri na kufanya maamuzi (conscious mind), kuna akili inayopokea na kutoa kila unachofikiri ila haifanyi maamuzi (subconscious mind), na kuna akili yenye kuongozwa kwa imani (super-conscious mind).
Katika mafanikio na hata imani nyingine sehemu kubwa inayoathiri maisha yetu ni subconscious. Akili hii haiwezi kutofautisha kati ya mema na mabaya, yenyewe inapokea kila kitu kinachoingizwa (kwa mfumo wa mawazo) na kutoa vitu hivyo katika maisha ya kawaida. Ndio maana mtu anayefikiria kuumwa kila mara hupata ugonjwa kweli. Mtu anayezungumzia ajali kila mara huishia kupata ajali. Na mtu anayefikiria mafanikio kila mara huishia kupata mafanikio. Hii ni kwa sababu akili hii huvuta yale ambayo unayafikiri kila mara na kuyaleta kwenye maisha yako.
Kama ni kufikiria tu mazuri kwa nini kila mtu hafanikiwi?
Kama tulivyoona ni kwamba akili hii inapokea chochote kinachowekwa, haiwezi kutofautisha mema au mabaya. Mawazo yakishaingia yenyewe inayafanyia kazi na kukuletea yale mazingira. Sasa inawezekana umeshawahi kufikiria sana kuhusu kufanikiwa na akili yako ikaanza kukutengenezea mazingira hayo, baadae ukaingiza tena mawazo ya kushindwa, au wasiwasi hivi nitaweza kweli, au kusikiliza wanaokukatisha tamaa kwamba huwezi. Akili yako inachukua mawazo haya pia na kuandaa tena mazingira ya kushindwa. Hivyo unajikuta huwezi kufikia mafanikio kwa sababu huna uhakika na kitu kimoja unachokitaka.
Nini kinatokea kwenye uchawi au imani nyingine?
Kwenye uchawi au imani nyingine kinachotokea ni kwamba mtu anaaminishwa kwamba kwa kitu fulani atakachofanyiwa ni lazima atapata mafanikio makubwa. Kwa mfano mtu anaambiwa ukiwa na hirizi hii utapata chochote unachotaka. Mtu huyu anatembea na hirizi yake akiwa na uhakika asilimia mia moja kwamba atafikia mafanikio anayotaka, na kweli inatokea hivyo. Kilichompa mafanikio sio hirizi ila ile imani yake na mawazo kwamba lazima atafanikiwa kitu ambacho angeweza kukifanya hata bila ya hirizi.
Kwa wale wafuasi wa dini kuna miujiza mingi sana inatokea kwenye dini na imewahi kutokea. Miujiza yote hii inatokana na imani za watu kwamba wanaweza kupona, wanaweza kufikia mambo makubwa.
Hapa nimegusia machache sana na kwa juu ili upate picha ya jinsi gani mambo haya yanakwenda, unaweza kuendelea kujifunza zaidi ili kupata elimu ya ndani sana. Lakini ukweli ndio huu tuliozungumzia hapa.
Wiki ijayo tutaona ni jinsi gani masharti wanayopewa watu kwa waganga yanaweza kuwasaidia kufikia mafanikio makubwa wakati waganga wenyewe wana maisha magumu.
Nakutakia kila la kheri katika safari ya kufikia mafanikio makubwa, usidanganywe kwamba uchawi ndio maajabu ya wewe kufanikiwa, maajabu unayo mwenyewe kwenye kichwa chako.
Makirita Amani
AMKA MTANZANIA: Je Uchawi Unaleta Mafanikio?
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments