[wanabidii] TAARIFA KWA WATANZANIA WANAOISHI OMAN

Monday, September 15, 2014

TAARIFA KWA WATANZANIA WANAOISHI OMAN


Ubalozi wa Tanzania nchini Oman unawatangazia Watanzania wote kuwa umeweka utaartibu maalum wa kushughulikia Watanzania wenye matatizo. Yafuatayo ni mambo ya kuzingatiwa:-

  1. Siku za kazi za ubalozi ni Jumapili hadi Alhamis kuanzia saa 2 na nusu asubuhi hadi saa 9 alasiri
  2. Kabla ya kuja Ubalozini piga simu kueleza matatizo yako na kama ikionekana kuna haja ya kuja ubalozini utapewa miadi ya kuja ubalozini wewe pamoja na bosi wako.
  3. Unapopiga simu hakikisha unazo mikononi taarifa muhimu kama vile, jina la bosi wako, namba yake ya simu, mnakoishi, umekuja lini Oman, namba yako ya simu, jina na namba ya simu ya wakala aliyekufanyia mpango wa kuja Oman.
  4. Jumanne ya kila wiki ndiyo siku maalum ya kushughulikiwa Watanzania wenye matatizo. Watakaohudumiwa ni wale tu waliopewa miadi.
  5. Ijulikane kwa wote kuwa Ubalozi hautoi huduma ya malazi kuwahifadhi Watanzania wenye matatizo, hivyo baada ya kuwasilisha matatizo yako utapaswa kurejea kwa bosi wako wakati matatizo yako yanashughulikiwa. Ubalozi pia hautoi fedha kuwasafirisha Watanzania kurudi Tanzania. Hili ni jukumu binafsi la mhusika.
  6. Namba za simu za Ubalozi ni: 24601174/24603373, piga namba hizi kuelezea matatizo yako na kuomba miadi.
  7. Ubalozi upo Muscat eneo la Madinat Al Sultan Qaboos Way No.2135, Nyumba namba 1798.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments