[wanabidii] MTOTO WA KIKE AKIPATA UJAUZITO AENDELEE NA MASOMO?

Friday, September 05, 2014

Kati ya mambo ambayo ni HATARI sana kwa watanzania ni kuhararisha MAZOEA kuwa SHERIA......

Hivi mpaka sasa umesikia na kushuhudia watoto wangapi wa shule za msingi na sekondari aidha Wamefariki wakiwa wanatoa mimba kama tokeo la kuogopa kufukuzwa shule au wameachishwa masomo kwa kosa la kupata UJAUZITO?

Ni kweli kuwa si maadili na si ruhusa kwa wanafunzi kujihusisha na tabia mbaya ukiwemo uzinzi.

Lakini je hawa watoto wa kike wakiachishwa masomo kuna utaratibu wa kuwaruhusu kuendelea na masomo?

Rejea hotuba ya Bajeti(2014/2015) ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi na Sera ya Elimu ya 2012(mchakatoni) ambayo ipo mbioni kupelekwa bungeni,inasema "SERIKLAI INAJITAHIDI KUMWONDOLEA VIKWAZO VYOTE MTOTO WA KIKE IKIWEMO KUENDELEA NA MASOMO AKIWA MJAMZITO NA BAADA YA KUJIFUNGUA" Swali ni je mazingira ya kumfanya aendelee na masomo akiwa mjamzito yapoje?

Ukweli ni kwamba hakuna sheria yoyote inayosema mtoto wa kike akipata ujauzito afukuzwe shule.......Kwa maana hiyo ipo haja ya kutafakari juu ya HAKI YA MTOTO WA KIKE ALIYEPATA UJAUZITO/ALIYEJIFUNGUA KUENDELEA NA MASOMO......

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments