JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA KAZI NA AJIRA
Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania
(TaES
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MIKAKATI YA WAKALA WA HUDUMA ZA AJIRA KUSAIDIA WANANCHI WA TANZANIA KUINGIA KATIKA USHINDANI WA SOKO LA AJIRA NCHINI
UTANGULIZI
Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) ulianzishwa kwa Sheria ya Wakala Na. 30 ya mwaka 1997 (kama iliyorekebishwa mwaka 2009) na kuzinduliwa rasmi tarehe 16 Juni, 2008 kufuatia Tamko la Serilkali Na.189 la mwaka 2008. TaESA ilianza rasmi utekelezaji wa shughuli zake tarehe 1 Julai, 2008 ikichukua nafasi ya kilichokuwa Kituo cha Ajira nchini (Labour Exchange Centre).
Wakala unatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Ajira ya mwaka 2008; Sheria ya Kukuza Ajira Na. 9 ya mwaka 1999 na Azimio Na. 88 la mwaka 1948 la Shirika la Kazi Duniani (ILO) ambalo Tanzania imeliridhia.
TaESA kwa sasa inahudumia wateja wake kupitia ofisi nne (4) za kanda ambazo ni Kanda ya Ziwa ambayo inahudumia mikoa ya Mwanza, Geita, Kagera, Simiwi na Shinyanga. Kanda ya Kaskazini ambayo inahudumia mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga. Kanda ya Kati ambayo inahudumia mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, na Kigoma. Kanda ya Mashariki na Pwani ambayo inahudumia mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Mtwara na Lindi.
1.0 MAFUNZO KWA WATAFUTAKAZI
Katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wahitimu wa kitanzania kwenye soko la ajira, Wakala umekuwa ukitoa mafunzo ya namna ya kushindania fursa za ajira. Mafunzo haya yamevutia watafutakazi wengi ambao tayari wako sokoni na walioko vyuoni. Aidha mafunzo haya yamewabadilisha vijana wengi waliohudhuria kuhusu suala zima la kuajiriwa na kujiajiri na kupelekea uhitaji wa mafunzo haya kuongezeka.
Kutokana na hitaji kuongezeka, TaESA imejipanga kutoa mafunzo haya kwa mwaka huu wa fedha kwa watafutakazi 2000 na kutembelea vyuo 20. Aidha kwa sasa Wakala umeshafanikiwa kutoa mafunzo kwa watafutakazi 2146, kati yao wanaume ni 1254 na wanawake ni 879. Vilevile Wakala umeweza kutoa mafunzo haya kwa vyuo vitano (5) ambavyo ni Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM), Taasisi ya Uhasibu (TIA), Chuo cha Ardhi na Taasisi ya Teknolojia (DIT), vyuo hivyo viko Katia mkoa wa Dar es salaam na kuhudhuriwa na wanavyuo 860, kati ya hao wanaume ni 513 na wanawake ni 347.
Kwa sasa mafunzo haya hutolewa kila Ijumaa kwa watafutakazi waliosajiliwa TaESA.
1.1 AINA YA MAFUNZO
Katika kutoa mafunzo haya tumekuwa tukitoa mada mbalimbali ili kuwasaidia watafutakazi kuweza kumudu ushindani kwenye soko la ajira. Mafunzo hulenga kuwajengea uwezo na ujuzi wa kuandika barua za maombi ya kazi, wasifu binafsi, jinsi ya kufanya usaili kwa kujiamini na kupata uelewa kuhusu matarajio ya waajiri kwa wafanyakazi. Vilevile kubadilisha mitazamo ya watafutakazi juu ya suala zima la kujiajiri na kutengeneza fursa mbalimbali za ajira kwa njia ya ujasiriamali.
2.0 HITIMISHO
Lengo la kuandaa taarifa hii ni kuujulisha umma kuhusu harakati za Wakala wa Huduma za Ajira katika kusaidia watafutakazi kushindania fursa za ajira.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments