[wanabidii] Meena akamatwa Dar kwa kujifanya Afisa Usalama wa Taifa

Wednesday, September 03, 2014
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI

JESHI LA POLISI TANZANIA

PRESS RELEASE
02/09/2014

ANAYEJIFANYA AFISA USALAMA WA TAIFA ANASWA DAR ES SALAAM

Mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kutokana na makosa mbalimbali ya kujifanya ni mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa. Mtu huyo anayejulikana kwa jina la GUNNER S/O SAIMON MEENA, Miaka 40, Mkazi wa Kinyerezi Segerea anatuhumiwa kuwasumbua wafanyabiashara mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa kuwasingizia au kuwatuhumu kwamba wanahusika na makosa yenye kuhatarisha usalama.

Kwa muda mrefu Jeshi la Polisi limekuwa likimtafuta mtu huyo kutokana na malalamiko mengi 
ambayo yamekuwa yakijitokeza na uchunguzi unaonyesha kwamba jina lake halipo katika orodha ya watumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Tukio la mwisho lililomfanya akamatwe ni pale alipomtishia mfanyabiashara mwenye asili ya kisomali aitwaye ABDI S/O MOHAMED DALMAR. Katika tishio hilo la kutishia mtuhumiwa GUNNER S/O SAIMON MEENA ambaye ni Afisa Usalama feki alidai apatiwe kiasi cha fedha za kitanzania TSHS 25,000,000/= (SHILINGI MILLIONI ISHIRINI NA TANO) ama sivyo angechukuliwa hatua chini ya sheria ya Usalama wa Taifa.

Mlalamikaji alitoa taarifa na ndipo mtuhumiwa akakamatwa katika mtego wa Polsi. Uchunguzi zaidi wa shauri hili unafanyika na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya jalada la kesi yake kupitiwa na mwanasheria wa Serikali.

S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments