Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumanne 5 Agosti 2014, Mjadala wa Bunge Maalum la katiba.
wadau, baada ya mapumziko ya zaidi ya miezi miwili, Bunge Maalum la Katiba linaendelea tena leo Mjini Dodoma. Jana tarehe 4 Agosti 2014, Kamati ya Uongozi ilikutana kujadiliana masuala kadhaa juu ya bunge hilo. Yapo masuala kadhaa waliyoafikiana kubwa zaidi ni kufanya marekebisho ya baadhi ya kanuni ili kuboresha mfumo wa kuendesha bunge hilo. Kuna kanuni 11 zitafanyiwa maboresho kwa siku ya leo. Nitawatajia hints za mambo mawili tu kutokana na umuhimu wake.
Ili kudhibiti tabia ya baadhi ya wabunge kuchukua posho (Per Diem) na kutohudhuria vikao vya Bunge, maboresho yatafanyika ili wabunge wa aina hiyo wasiwe na haki ya kuchukua posho. Kwa utaratibu wa awali ni kwamba wabunge wote walipewa Perdiem ila kwa wale ambao walikuwa hawahudhurii vikao walikuwa wanakosa posho za vikao tu. Hali hiyo itaokoa fedha nyingi ambazo zilikuwa zinapotea kwa wabunge wasiofanya kazi za Bunge Maalum kutokana na sababu mbalimbali.
Marekebisho mengine yatahusu utaratibu wa mijadala ya Sura za Rasimu. Kwa mujibu wa Kanuni, Bunge linajadili sura mbili mbili. Hata hivyo, marekebisho yatafanyika ili Bunge lijadili sura zote 15 zilizobaki kwa pamoja kwa utaratibu ufuatao;
Wabunge watajadili sura zote 15 ndani ya Kamati 12 za Bunge Maalum. Zoezi hilo litafanyika kwa siku 15 kuanzia kesho tarehe 6 Agosti 2014
Baada ya mijadala ndani ya kamati kukamilika, Kamati zitapewa siku 3 kuandika taarifa za kamati kwa sura zote 15
Baada ya Kamati kukamilisha taarifa za Kamati, Kamati hizo zitawasilisha ndani ya bunge hilo taarifa zake na zoezi hilo linatarajiwa kuchukua siku 5.
Baada ya kamati kukamilisha uwasilishaji wa Taarifa, Mijadala juu ya Sura hizo itaanza.
Mijadala ikikamilika Bungeni, Kamati ya Uandishi itaandika Sura zote kwa kuzingatia maoni ya taarifa za kamati na mijadala bungeni
Kamati ya Uandishi itawajibika Kuwasilisha Bungeni Mpangilio wa sura baada ya maobresho. Wabunge watazipitia tena na kufanya marekebisho stahiki.
Baada ya Bunge kukubaliana na kazi ya Kamati ya Uandishi, ndipo zoezi la upigaji kura litafanyika. Kwa hali hiyo, Sura zote zitapigiwa kura kwa pamoja mwisho wa Bunge hilo.
kazi kubwa kwa siku ya leo itakuwa kurekebisha kanuni hizo na inatarajiwa kuwa zoezi hilo litakamilika ndani ya siku moja. Kuanzia kesho, Bunge Maalum litaendelea vikao vyake ndani ya Kamati kwa siku 15. Kama kawaida mimi pamoja na wadau wengine tutawaletea moja kwa moja mijadala ya Bunge Maalum kama itakavyojitokeza Mjini Dodoma. Natarajia ushirikiano kutoka kwa wadau wote ambao tulikuwa nao kuanzia Februari 18 mwaka huu.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments