[wanabidii] WIZI MPYA COCO BEACH

Saturday, August 16, 2014

Wizi huu hufanywa na vibinti vinavyovutia sana, na wanaume tu ndio huibiwa, hivyo akina mama tafadhali muwambie waume zenu na maboifrend wajihadhari. Wizi huu hutokea kule baharini maeneo ya Koko, ukipaki tu vibinti viwili vizuri huja na kuanza kusafisha kioo cha gari lako, wakati wakifanya hivyo hujiachia viblauzi na visidilia vyao unajikuta huwezi kuacha kukodolea macho. Vikimaliza usafi husema havihitaji malipo ila vinaomba lifti kwenda Msasani. Ukikubali vinapanda kiti cha nyuma na kuanza kukushika shika shingo na masikio, kamoja kanahama kiti na kuja kiti cha mbele na kuanza kukula denda wakati kenzie kanakuibia mkwanja wako. Bosi wetu kaibiwa juzi, jana tena kaibiwa na leo keshatupigia simu kuwa kaibiwa, na kesho ni wazi ataibiwa. Tunaomba mjihadhari sana

Aksante

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments