Katika zama zote tangu uhuru, Tanzania imekuwa ikiongozwa na chama cha Mapinduzi.Tunasema tangu uhuru kwa sababu Tanzania ni matokeo ya muungano kati ya Tanganyika na Zanzbar, na kabla ya mwaka 1977, tulikuwa na TANU kwa Tanganyika, ASP kwa zanbar , vyama ambavyo viliungana na kuizaa CCM, hivyo tunaweza tukasema CCM ya 1977, ilikuwa ni muendelezo tu wa ASP na TANU katika sura mpya hivyo kilikuwa ni kitu kile kile.
Katika kipindi chote ambacho Chama cha mapinduzi kimekuwa kikiiongoza Tanzania, kimefanya mengi mazuri na kimeonesha madhaifu vile vile.Katika mazuri ambayo kimefanya miongoni mwa mengi, ni pamoja na kupanua wigo wa kupata elimu kwa watanzania, kuboresha miundombinu, kuboresha afya, kujenga wigo mkubwa wa demokrasia kwa kiasi cha kuonekana kimataifa kama nchi inayokuwa katika eneo la demokrasia n.k. Hata hivyo, kwa kuwa maendeleo ni mchakato, na sio tukio bado Uchumi na hali ya kimaisha ya mtanzania pamoja na upatikanaji wa huduma mbali mbali za kijamii, bado ni duni kuashiria kwamba juhudi zaidi zinahitajika katika kuleta maendeleo ya watu.
Pamoja na mengi mazuri, ambayo chama cha mapinduzi kimeyafanya katika nyakati zote, pia kimeonesha madhaifu kadha wa kadhaa. Udhaifu ambao umekuwa ukizungumzwa sana hasa na watanzania wenyewe, ni kuhusu Chama cha mapinduzi kushindwa kuzuia rushwa kubwa kubwa serikalini (Grafts) na rushwa ndogo ndogo (bribes), rushwa ambazo kwa kiwango kikubwa zimekuwa zikidumaza maendeleo na kuleta ufanisi duni katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Kumekuwa na mitizamo ya aina mbili kuhusu muelekeo wa CCM na jinsi ilivyoweza kuisimamia serikali kwa kipindi chote.Mtizamo wa kwanza ni wale wanaofikiri kwamba pamoja na mapungufu ya chama cha mapinduzi,kuna mengi mazuri ambayo chama kimeyafanya na chama cha mapinduzi bado ndicho chama bora Tanzania ukilinganisha na vyama vingine vilivyopo Tanzania na hawa hufikiri kwamba matatizo yanayotokea ndani ya CCM, ni matatizo ya kibinadamu, na ni matatizo ambayo yanatokana na tabia za watu tu na si ya kisera.Wenye mtizamo huo, wanaamini kwamba madhaifu ya CCM yanaweza kushughulikiwa kwa kukosoana wenyewe kwa wenye pamoja na kukosolewa na vyama vya upinzani lakini si zaidi ya hapo maana hata ukiangalia katika vyama vingine, matatizo kama vile rushwa na upendeleo mahali pa kazi/ndani ya vyama kwa mfano,n.k yapo japo kwa viwango tofauti tofati, hivyo kundi hili huamini kwamba, matatizo mengi yanatokana na jamii yenyewe na si chama kama Taasisi.
Kundi la pili, ni lile linaloamini kwamba, kutokana na udhaifu waliouonesha CCM katika kipindi chote cha utawala wao, hakuna sababu ya kulinganisha mazuri na mabaya waliyoyafanya ila kwao jambo la msingi ni kutafuta udhaifu na kisha kutumia udhaifu huo kukiondoa chama cha mapinduzi madarakani.Wengi katika kundi hili hutokana na wale wanaodai kuwa ni vyama vya upinzani.
Kwa kuwa kundi hili linadodai kuwa ni la vyama vya upinzani ni kundi la watafuta madaraka, haifai kulaumiwa kwa kutafuta mbinu za kuing'oa CCM, kwa kuwa ni kwa kupitia njia hiyo tuu, wanaweza kufikia lengo lao, lakini kwa hoja ya udhaifu wa Chama cha mapinduzi pekee si sababu ya kutosha kuvichagua vyama vingine kwa kuwa kwanza inafaa kufahamu udhaifu uko kwenye eneo gani na unasababishwa na nini na vyama hivyo vinavyodai kuwa vya upinzani vinakuja na mbinu gani ya kukabiliana na udhaifu husika kwa nadharia na matendo na kinyume chake hakuna kitu.
Kwa bahati mbaya ni kwamba, mpaka sasa, hakuna chama chochote cha upinzani Tanzania ambacho kimeweza kuainisha kinagaubaga chanzo hasa cha matatizo ya CCM na serikali yake kama vile rushwa, ahadi zisizotekelezwa kikamilifu n.k na kuja na njia mbadala ya kitaalam inayotekelezeka na kuanza kutekeleza angalau katika ngazi ya vyama vyao, kinyume chake, vyama hivyo vimekuwa ni vyama vya kulaumu tu, kuzua, kusema uongo uongo, kufanya uchochezi, kugomagoma, kupinga pinga kuhamasisha uvunjaji wa sheria na kadhalika huku vikiwa havina mikakati ya kinadharia na kimatendo inayoelekeza ni kwa namna gani vinaweza kushughulikia matatizo sugu yanayoikabili Tanzania na bara la Afrika.
Vyama vya upinzani vimekuwa vikihamasisha watu kukikataa chama cha Mapinduzi kwa hoja ya kwamba kimeshindwa lakini vyenyewe havielezi vinaweza nini, vinawezaje, na vinathibitisha je kwamba vinaweza.Kadhalika wanachama wa vyama hivyo wamekuwa wakisema kwa kukariri kwamba wamekichoka chama cha mapinduzi, hivyo wao wanajiunga na watachagua, na wanataka watanzania wachague vyama vya upinzani, jambo linaloashiria kuwa, watu hao wamejiunga na vyama vya upinzani kwa sababu tu ya kuchoshwa na CCM, lakini si kwa ubora wa vyama vya upinzani vyenyewe.
Watanzania waliowengi, wenye fursa ya kutafakari na kuchanganua mambo, hawawezi kuamua kwa hiari yao kuruka Majivu na kukanyaga moto huku wakiwa wanaona. Wapinzani wa Tanzania wanaodai kwamba wamejiunga na watachagua upinzani kwa kuwa wameichoka CCM, ni sawa na mtu aliyemchoka mume/mkewe kwa kuwa kakaa naye muda mrefu na amekuwa akionesha udhaifu wa kibinadamu mara kwa mara, na akaamua kwenda kuokata mwanamke yeyote mtaani , si kwa kuwa aliyemwokota ni mke/ mume mwema, la hasha! Kwa kuwa tu kamchoka mke/mume wake wa awali.
Kutokana na Vyama vya upinzani kutokuwa na misingi imara nay a kweli ya kihoja na kiuadilifu ya kusimamia, ni wazi kwamba CCM itaiongoza tena Tanzania kwa miaka mingine hamsini (50) ili kufikisha Karne moja. Hata hivyo umuhimu wa uwepo wa vyama vya upinzani Tanzania bado unaendelea kuwepo kwa kuwa vyama hivyo vimekuwa vikikosoa na vitaendelea kukikosoa chama cha mapinduzi na kukifanya kuzinduka pale kinapoteleza, lakini si kuongoza nchi kwa kuwa uwezo na ubora wa vyama hivyo haukaribii hata kwa mbali uwezo wa chama cha mapinduzi, na watu wanaounda vyama vyote wanatoka kwenye jamii ile ile na wana tabia na mitizamo ile ile.Yaani kama ni magari, unaweza kusema vyama vya upinzani Tanzania ni sawa na duet, wakati Chama cha mapinduzi ni sawa na Range Rover Sports.
Tukitakie chama cha mapinduzi kila la heri katika kuiongoza Tanzania kwa miaka mingine hamsini (50).
Malcom Kazindogo Shaw,
Professor of International Maritime Law,
University of Brunei Du Daru'salaam
Brunei.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments