[wanabidii] USHAURI WA DADY IGOGO KWA WANAOTAKA KUGOMBEA UONGOZI BAVICHA

Wednesday, August 13, 2014
KUELEKEA BAVICHA. 
(Kwanza - sigombei)
Ni hatari kwa chama kupata Kiongozi wa Taifa wa BAVICHA ambaye hana rekodi au uzoefu wowote wa uongozi wa ndani ya chama, wala hajawahi kushika nafasi ya ngazi ya msingi au tawi. Tunapoelekea kwenda kuchukua dola hatupaswi kufanya rehearsal ya uongozi muhimu wa juu kabisa kama nafasi ya Mwenyekiti wa BAVICHA. Hatupaswi kufanya majaribio ya nafasi muhimu kama Mwenyekiti ambaye atakuwa ni mjumbe wa kamati kuu ya chama, baraza kuu na mkutano mkuu kwa cheo chake. Hapaswi kuwa na rekodi ya usaliti ndani ya chama. Hapaswi kuwa na rekodi ya rushwa ndani ya chama, hapaswi kuwa mpenda makundi ndani ya chama, hapaswi kuwa amejitafutia umaarufu kwa kuattack personalities! Awe na rekodi ya uaminifu isiyo na shaka. Awe anafahamu ngazi za chini na matatizo ya vijana wa vijijini bali siyo lower and upper middle class pekee yake za Twitter, Instgram, FB na Jamii forum. NITAMPINGA YEYOTE AMBAYE ATAKUWA NA SIFA HIZO. WATU TUMEKAA JELA TUKIWA NA VITANDA VIZURI, TUMEPIGWA BARIDI TUKIWA NA BLANKETI, TUMELALA NJAA TUKIWA NA MAVUNO MENGI, TUKAKOSA FURSA ZAIDI KWA SABABU ZA BAVICHA. Tulianza kuijenga Bavicha kabla haijaanza bado ikiwa ni Kurugenzi ya Vijana 2006 nikiwa na Mnyika, Kinabo, Regia, Killian Nango, Kafulila.... Tuliandika Katiba ya Bavicha, Tulikesha kuandika Sera ya vijana, tulikesha na kukeshaaaaaaa....tukaanza kwenda Field... Leo watu wanataka Uenyekiti kwa kutumia IPad akiwa chumbani kwake na hawara yake akipost FB... Leo mtu anataka Uenyekiti haijui ngazi ya msingi zaidi ya kuisoma na kuinukuu kwenye Katiba... anataka Uenyekiti.... Bavicha ni zaidi ya FB na JF... ni zaidi ya comments na likes!!! ni zaidi ya kuomba muongozo kwa moderates u guys!! Ni taasisi imara... ni zaidi ya socio-media... ni zaidi... JITAFAKARINI KWA KINA SANA....

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments