[wanabidii] Tuendelee kuliona Taifa la Uchina likizidi kuwa kimya na kunyamazishwa kabisa

Friday, August 22, 2014
Pamoja na China kuwa imara sana kiuchumi mpaka sasa imekua nchi ya pili yenye uchumi mkubwa na imara Duniani nyuma ya Marekani na pia kuwa na nguvu kubwa ya kijeshi lakini China imekosa sauti dhidi ya mataifa ya magharibi. Sasa hivi China hana sauti mbele ya mataifa ya magharibi pindi unapojitokeza mgogoro unaohitaji sauti za mataifa makubwa kukemea, China ilijaribu kufanya hivyo kwenye mgogoro wa Syria lakini muda mfupi baadae China ikanyamaza kabisa, ilijaribu pia kuweka sauti kwenye mgogoro wa Iran nako pia ikanyamaza, kwenye mgogoro wa Russia na Ukraine mataifa mengi yalitegemea China itatoa support kubwa kwa MSocialist mwenzake Russia lakini China imekuwa kimya kama haipo vile. Sababu kubwa zinazopelekea China kutojihusisha kabisa na hii migogoro ni ukweli kwamba umoja wa taifa la China upo katika hali mbaya sana China kama China ina migogoro mingi sana ya ndani ambayo inahitaji diplomasia ya hali ya juu kukabiliana nayo, China imegundua haipaswi kujihusisha na mgogoro wowote ule ambao utachafua hali ya hewa. Jimbo la Tibet linataka kujitenga kutoka China na Tibet inapewa support kubwa na Nchi za magharibi na Tibet wapo tayari muda wowote ule kuhasi, Taiwan kama milki ya China nayo ina mgogoro wa muda mrefu sana na serikali ya Beijing, Taiwan awali ndio ilikua imebeba roho ya Uchina na makao makuu ya China zamani yalikua kwa serikali ya Taiwan, Taiwan wapo vizuri sana kwa viwanda na technology na Taiwan sio tena ya kisocialist na kila siku wanahitaji kujiondoa kwenye utawala wa serikali ya Beijing na China haitaki kuiachia Taiwan kwa kuhofia kuporomoka kiuchumi, wapo tayari muda wowote kupigana vita. Hong Kong nayo kama jimbo la China ambalo sera zake nyingi ni za kicapitalist nao wamekuwa wakitaka kujitangazia mamlaka kamili, kuondoka kwa jimbo hili bila shaka kutakua hakuna tena uimara wa China. Ikumbukwe pia sasa hivi China imezungukwa na mataifa yenye mlengo wa kicapitalist mfano Tiger economy countries kama Thailand, Singapore na Malaysia, pia imezungukwa na washirika wa Marekani ambao ni Japan na South Korea. China imebaki na North Korea tu kama ndio mshirika wake mkubwa. Pia China ana mgogoro wa kudumu na jirani yake Japan wa kugombea visiwa ambavyo ni muhimu sana kwa uzalishaji wa gesi na nuclear nchi hizi mbili zilishapigana vita kwaajiri ya hivi visiwa na sasa zinatishiana tena kupigana vita na ikumbukwe Japan ni mshirika mkubwa wa Marekani hua wana ushirika wa kiuchumi na kijeshi, pia marekani kwenye huo ukanda wana Military base pamoja na vituo vya makombora ya kujihami, hivyo kwa vyovyote vile China itaathirika sana na vita yoyote ile itakayotokea. Pia baada ya China kutafuta washirika wengine mbali na wale wa ukanda wake ambao tayari wametekwa na nchi za magharibi China walikuja moja kwa moja kuwekeza Africa na kuifanya Africa kuwa mshirika wake kiuchumi, kisiasa na kijeshi lakini napo Marekani wameingilia kati ili kuondoa uwekezaji wa China kwa Africa na kupenyeza ubepari wao, juzi tulishuhudia viongozi wa Africa wakipata mualiko wa ikulu ya White house ili kukaribisha uwekezaji mkubwa wa Marekani kwa Africa. Ziara ya Rais Obama Africa ilikua ni katika nchi zenye ushawishi kwa mataifa mengine na zenye maeneo mengi ya uwekezaji na ziara hiyo ilikua ni kwa kanda 3. West Africa alikwenda Senegal, South alikwenda S.Africa and East Africa alikuja Tanzania. Hakwenda North kwavile tayari alishajipenyeza baada ya kuuangusha utawala wa Kanal Muamar Gadaf na kuidhoofisha Egypt ambayo ilikua ndio moyo wa mataifa ya kiarabu ya Mashariki ya Kati. Marekani anafanya kila jitihada ili tu utawala wa kisocialist usijipenyeze popote pale wala kuimarika na amefanikiwa sana kwa hilo toka alipousambaratisha utawala wa USSR, pia vita ya Vietnam ambayo lengo kuu ilikua ni kuzuia usocialist usisambae kutoka mataifa ya kaskazini kuja kusini ambao ulikua ukikua kwa kasi na kuenea, amefanikiwa kwa vile usocialist ulikomea North Vietnam. Kurudi kwa ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Cuba pamoja na kifo cha Hugo Chavez ni sababu zilizochangia sana kudhoofisha ushirikiano wa mataifa ya Kisocialist na ukuwaji wa socialist countries. So baada ya hayo tuendelee kuliona Taifa la Uchina likizidi kuwa kimya na kunyamazishwa kabisa.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments