TAMKO LA NDUGU ERNEST E. SHESHE
ALYEKUWA MWENYEKITI WA CHADEMA
WILAYA YA ARUMERU MAGHALIBI 26
AGOST 2014.
Ninaitwa Ernest Sheshe. Nilikuwa
Mwenyekiti wa CHADEMA katika Jimbo la
Arumeru Magharibi kuanzia mwaka 2009
hadi tarehe 25 Agosti 2014.
1. Niligombea nafasi ya uenyekiti tena katika
uchaguzi wa chama unaoendelea.
Nilishindwa kwa hila na Ndugu Gibson. Hila
zenyewe ni pamoja na Mhe. Godless Lema
kuwahonga wajumbe wa mkutano mkuu wa
Jimbo shilingi 30,000/= kila moja na kisha
kuwaficha hadi siku ya uchaguzi. Aidha,
wajumbe walipelekewa chakula mafichoni
kilichobebwa kwenye gari ya mgombea
mwenzangu, yote haya ikiwa ni kinyume na
kanuni za uchaguzi ndani ya chama na
Waraka Na.6 uliotolewa na Katibu Mkuu.
Waraka huu, pamoja na mambo mengine,
unapiga marufuku matumizi ya hongo ya
aina yeyote katika chaguzi.
2. Siku moja kabla ya uchaguzi, Mhe.
Godbless Lema aliwatangazia wanachama
kwamba Mwenyekiti wao ni Gibson na ndiye
atakayekuwa mgombea ubunge. Wagombea
wengine wanaojipitisha ni mamluki na ni
wasaliti wa chama na wananchi wa Arumeru.
3. Baada ya kutoridhika na matokeo ya
uchaguzi kutokana na matukio ya hapo juu,
nilikata rufaa kwa kuandika barua kwenye
ngazi ya mkoa kama utaratibu unavyosema.
Hata hivyo barua yangu ya rufaa ilipelekwa
kwa Katibu wa Kanda Ndugu Amani
Golugwa, ambaye ndiye aliyesimamia
uchaguzi. Ndugu Golugwa ametamka wazi
kwamba hakuna cha rufaa wala nini na
kwamba yeye hajishughulishi na wasaliti na
kwamba hiyo imetoka!
4. Mambo mengine yanayoendelea ndani ya
chama katika Kanda ya Kaskazini ni:
a. Uongozi wa kanda hauko kikatiba na
unafanya kazi kwa kuvunja katiba ya CDM
b. Mjumbe wa kamati kuu Godbless Lema
ametengeneza chama ndani ya chama.
Yeyote asiyekubaliana naye na asiye na hela
hana thamani ndani ya chama. Nguvu yote
hii ya Lema anaipata kutoka kwa mwenyekiti
wa CDM taifa Freeman Mbowe kutokana na
kwamba ni kabila lake.
c. Mhe. Godbless Lema ndiye anayepanga
nani awe Kiongozi ndani ya chama na ndiye
mwenye mamlaka ya kuamua nani
atagombea ubunge katika uchaguzi ujao kwa
majimbo ya Mkoa wa Arusha.
d. Katibu wa kanda Aman Gulugwa ni tatizo
kubwa ndani ya CDM,anapenda kuburuza
watu,hafuati katiba wala kanuni za
uendeshaji wa chama.
5. Baada ya kutafakari hali ya mambo
inavyoendelea ndani ya CDM, na kujiridhisha
kwamba chama hiki kimetekwa na viongozi
wachache na kuachana kabisa na misingi
tuliokuwa tunaijenga, na kutokana na
ukandamizaji wa demokrasia unaoendelea,
nimeamua rasmi kujiunga na chama kipya
kinachoitwa ACT_Tanzania ambacho viongozi
wake ni waadilifu na baadhi yao pia
wamedhulumiwa haki zao ndani ya CDM.
Kunzia tarehe tarehe 26 Agosti 2014 siku ya
Jumanne mimi sio mwanachama na kiongozi
wa CDM tena. Ninajiunga na wazalendo wa
ACT-Tanzania.
6. Pamoja nami, tupo na wazalendo wengine
14 kutoka kata 14 za Jimbo la Arumeru
Magharibi. Kuanzia kesho kutwa tutaanza
kukisimika chama cha ACT-Tanzania katika
kata zote za Arumeru Magharibi na
tutashiriki kikamilifu katika uchaguzi wa
serikali za mitaa kadri utakavyopangwa.
Ndimi Ernest E. Sheshe,
Mwanachama wa ACT-Tanzania,
Arumeru Magharibi.
-- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments