Serikali fanyeni hili laweza kuwa dawa kwa masomo ya sayansi.
Kumekuwepo na malalamiko mengi toka kwa wadau wa elimu ikiwemo serikali pamoja na wanafunzi kuhusiana na upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi.Serikali imejitanabahisha kuchukua hatua katika kuondoa tatizo hili bila mafanikio kwa sababu ya kufata njia isiyo sahihi yawezekana kwa kujua ama kutokujua.
Serikali imekuwa na utaratibu wa kutoa kipaumbele kwa kuchukua waliohitimu kidato sita na nne katika michepuo ya sayansi japo wenye ufaulu mdogo mno na kuwapa kozi fupi fupi ili wakawe walimu wa sayansi katika shule zetu za msingi na sekondari.Hili limeongeza walimu wa masomo hayo ila wasio na tija kwa kuzingatia uwezo wao..wanachokifanya walimu hao leo hii ni kuwakaririsha wanafunzi majibu ya mitihani mingi iliyopita ili wajibu mitihani yao na kufaulu na mwisho wa siku tunapata waliofaulu bila uelewa wa masomo husika.Huku tukijisifia kuwa ufaulu umepanda kwa asilimia kadha wa kadha na mbwembwe nyingiii tukiwataja walioongoza masomo ya sayansi na kuwapa zawadi nazoweza ita za kinafiki…
Naishauri serikali kupitia kwa wizara ya elimu iangalie uwezekano wa kufanya haya:-
1. Kuchukua wahitimu wa kidato cha nne na sita wenye ufaulu mkubwa na kuwaandaa kwa fani mama kama ualimu,udaktari,na uhandisi .
2. Kuchukua wahitimu wa vyuo vikuu kuanzia angalau mwaka 2008 mpaka leo,kwa fani za uhandisi ambao wamekuwa ni wengi mtaani bila kazi huku wakiwa na ufahamu mkubwa wa masomo ya sayansi lakini wamebaki kuwa washabiki wa wanasiasa. Waandaliwe kwa kuwajenga kifikra na kuwaboreshea maisha endapo wataenda ktk fani hizo tajwa.
3. Kuboresha maisha ya walimu waliopo sasa na kuimalisha usimamizi katika utendaji kazi wao.Ikiwemo kuwapa marupurupu mbalimbali ikiwemo teaching allowance.
4. Kuhakikisha kuwa waratibu elimu wanaoteuliwa ni watu makini ambao wanameonesha utendaji uliotukuka katika nafasi zao za awali kabla ya uteuzi.
5. Kuweka mfumo mzuri wa elimu ikiwemo mtaala na vitendea kazi vya kutosha mashuleni.
Kuweka malengo ya sasa na ya wakati ujao na kuyasimamia kuhakikisha yanafikiwa na yasipofikiwa kuwawajibisha wahusika….n.k
-- Kumekuwepo na malalamiko mengi toka kwa wadau wa elimu ikiwemo serikali pamoja na wanafunzi kuhusiana na upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi.Serikali imejitanabahisha kuchukua hatua katika kuondoa tatizo hili bila mafanikio kwa sababu ya kufata njia isiyo sahihi yawezekana kwa kujua ama kutokujua.
Serikali imekuwa na utaratibu wa kutoa kipaumbele kwa kuchukua waliohitimu kidato sita na nne katika michepuo ya sayansi japo wenye ufaulu mdogo mno na kuwapa kozi fupi fupi ili wakawe walimu wa sayansi katika shule zetu za msingi na sekondari.Hili limeongeza walimu wa masomo hayo ila wasio na tija kwa kuzingatia uwezo wao..wanachokifanya walimu hao leo hii ni kuwakaririsha wanafunzi majibu ya mitihani mingi iliyopita ili wajibu mitihani yao na kufaulu na mwisho wa siku tunapata waliofaulu bila uelewa wa masomo husika.Huku tukijisifia kuwa ufaulu umepanda kwa asilimia kadha wa kadha na mbwembwe nyingiii tukiwataja walioongoza masomo ya sayansi na kuwapa zawadi nazoweza ita za kinafiki…
Naishauri serikali kupitia kwa wizara ya elimu iangalie uwezekano wa kufanya haya:-
1. Kuchukua wahitimu wa kidato cha nne na sita wenye ufaulu mkubwa na kuwaandaa kwa fani mama kama ualimu,udaktari,na uhandisi .
2. Kuchukua wahitimu wa vyuo vikuu kuanzia angalau mwaka 2008 mpaka leo,kwa fani za uhandisi ambao wamekuwa ni wengi mtaani bila kazi huku wakiwa na ufahamu mkubwa wa masomo ya sayansi lakini wamebaki kuwa washabiki wa wanasiasa. Waandaliwe kwa kuwajenga kifikra na kuwaboreshea maisha endapo wataenda ktk fani hizo tajwa.
3. Kuboresha maisha ya walimu waliopo sasa na kuimalisha usimamizi katika utendaji kazi wao.Ikiwemo kuwapa marupurupu mbalimbali ikiwemo teaching allowance.
4. Kuhakikisha kuwa waratibu elimu wanaoteuliwa ni watu makini ambao wanameonesha utendaji uliotukuka katika nafasi zao za awali kabla ya uteuzi.
5. Kuweka mfumo mzuri wa elimu ikiwemo mtaala na vitendea kazi vya kutosha mashuleni.
Kuweka malengo ya sasa na ya wakati ujao na kuyasimamia kuhakikisha yanafikiwa na yasipofikiwa kuwawajibisha wahusika….n.k
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments