[wanabidii] Rais Kikwete kuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano wa Diaspora

Thursday, August 14, 2014
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika mkutano wa Watanzania wanaoishi ughaibuni (Diaspora) ambao umepangwa kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam tarehe 14 na 15 Agosti 2014.

Mkutano huo ambao umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taasisi ya Diaspora Tanzania (Tanzania Diaspora Initiative-TDI), unalenga kuwahamasisha Watanazania wanaoishi ughaibuni wenye utaalamu na mitaji kurudi nchini au kuwekeza katika shughuli mbalimbali kwa madhumuni ya kukuza uchumi wa nchi.

Aidha, Mkutano huo ambao ni wa kwanza kufanyika nchini, wenye kaulimbiu "Unganisha, Shiriki, Toa taarifa na Wekeza" (Connect, Engage, Inform and Invest) utatoa nafasi kwa washiriki kutambua vyema fursa za uwekezaji na ajira zinazopatikana Tanzania. 

Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es salaam

13 Agosti, 2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments