[wanabidii] MTANDAO WA WANAFUNZI WALAANI KUKAMATWA KWA VIONGOZI WA TAHLISO

Saturday, August 16, 2014
MTANDAO WA WANAFUNZI NCHINI TSNP UNALAANI VIKALI JUU YA KUKAMATWA KWA WANAFUNZI NA VIONGOZI WA JUMUIYA NA SERIKALI ZA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU TANZANIA.

waliokamatwa- Mwenyekiti TAHLISO-Mussa Mdede, Mhazini TAHLISO, Spika wa DIT, Raisi wa IFM, na wanafunzi wengine.

Chanzo: Kuratibu maandamano ya AMANI ya kudai Fedha za Mafunzo kwa vitendo" FIELD" ambazo hawajapewa tangu kuanza kwa FIELD Kinyume na ratiba. viongozi hawa wamechukua jukumu la kupaza sauti za wanafunzi waliopangiwa mbali mbali kufanya field bila ya kupewa fedha husika.

Mtandao huu ukiongea na baadhi ya viongozi waliokamatwa, Ndugu Mussa Mdede ambaye ni mwenyekiti wa TAHLISO-Jumuiya ya serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania na wengineo. umepata sababu za wao kukamatwa na kuwekwa Sero Kituo cha Polisi Ostabey. jijini Dar es salaam.

"Ni kwa takribani miezi miwili sasa tangu wanafunzi tuende FIELD hatujapewa fedha zetu za mafunzo kwa vitendo, sisi kama viongozi tunapigiwa simu jinsi wanafunzi wenzetu waliotupa dhamana ya kuwaongoza na kuwatetea wanavyopatashida, wanavyoishi maisha ya shida na kupelekea kutotimiza wajibu wao.

Taarifa ambazo TSNP imepata hivi karibuni ni kwamba, baadhi ya viongozi husika wameachiwa kwa dhamana ya kujidhamini wenyewe na sharti la kuripoti polisi J.3.

Viongozi wa mtandao huu wa wanafunzi tumekuwa tunapigiwa simu za mara kwa mara juu ya malalamiko dhidi ya serikali kutowadhamini fedha husika.hata hivyo sauti hizi zimesikika katika mikoa mbali mbali kama vile Dar es salaam, Arusha, Dodoma, Mbeya, Morogoro, Mwanza nk....

TUNAIOMBA SERIKALI IWAJIBIKE MAPEMA KABLA YA WANAFUNZI HAWAJAFIKIA HATUA YA KUANDAMANA KAMA ILIVYOPANGWA ILI KUDUMISHA AMANI NA UPENDO BAINA YETU.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments