Salaam
Ndugu zangu, napenda kutoa maoni yangu ya kile kinachotokea katika Kanisa la Moravian Tanzania.
Awali ya yote napenda niweke wazi kwamba mimi ni mmoja kati ya watu tulioshuhudia umwagaji damu na uharibifu mkubwa wa mali ukitoa watu kufa wakiwa magerezani kati ya mwaka 1991 na 1993 nikiwa darasa la sita Kijiji cha Bujonde Wilayani Kyela.
Ndugu zangu, ilikuwa vita kweli. Vile ilivyotokea Rwanda mwaka 1994 ilinikumbusha jinsi tulivyotaabika. Tulishinda kando ya mto kiwira na mashambani kukimbia yaliyokuwa yanatokea. Nakumbuka watu wakiwa na mapanga na mikuki wakiranda nyumba hadi nyumba usiku wa manane.
Kwa wakati ule, nina imani kwamba watanzania walio wengi hawakujua nini kilikuwa kinajiri kwani vyombo vya habari vilikuwa haba.
Kwa watanzania wapenda amani na wacha Mungu wa kweli. Hali hii inarudisha maumivu ya uhasama ambayo jamii ilianza kuyasahau. Wanaoumia ni wananchi kama ilivyokuwa 1992.
Ombi langu kwa viongozi wa Kanisa la Moravian ni kutathmini kwa Miono ya kweli kile kinachotokea.
Kwa Serikali yetu, naomba hatua za awali kuepusha kile kilichotokea mwaka 1991/1992 zichukuliwe.
Salaam kutoka Dodoma.
0 Comments