[wanabidii] Magufuli hata barabara za mitaa zinahitaji lami pia

Wednesday, August 27, 2014
Wakati wa mkoloni barabara za oysterbay kule dar na isamilo huko mwanza zilikuwa zimenakshiwa kwa lami kwani wakuu wa dola mabalozi na ma ceo waliishi huko.

Baaada ya uhuru hizi barabara sio tu ziliachwa hata ile lami iliyoachwa na mkoloni haipo badala yake tunaweka lami barabara za chato namtumbo kartesh gairo ambazo hata magari hakuna na yaliyopo yanaishia kukanyaga watoto wa shule mifugo na wapanda baiskeli ndo maana zikikamilika wananchi wanaandamana kudai matuta.

Kuna tatizo gani tukiweka lami mitaa ya mikocheni mlalakua masaki mbezi beach ambako ma ceo mabalozi na mawaziri wanaishi?

Haingii akili ma ceo wa crdb tbl nssf ppf tanapa tpdc ambao wana mchango mkubwa katika kufanikisha ulipaji kodi na budget ya nchi halafu barabara za kuchepuka kuelekea majumbani kwao ni mbovu. Nasikia hata barabara ya kwenda nyumbani kwa magufuli haina lami.

Fikiria kijana anaelipa kodi laki nane hadi milioni kwa mwezi anaishi makongo juu au msewe kila siku anabadili shokapu na ball joint za virtz yake kwa ubovu wa barabara, atakuwa na hamu ya kulipa kodi kweli?

Ifike sasa tuweke uwiano wa huduma za jamii kulingana mahitaji na uwiano wa watu, tukiamua kujenga barabara ya lami tuangalie na uhitaji, je hiyo barabara inatumika kwa wastani wa magari mangapi kwa saa au siku ni aina gani ya magari yanayotumika kule.
----------
Sent from my Nokia phone

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments