[wanabidii] KUKITHIRI KWA VITENDO VYA UJAMBAZI MKOANI KIGOMA

Friday, August 22, 2014
Ndugu zangu,
Kama ambavyo vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti juu ya matatizo makubwa tunayopata mkoani kwetu juu ya kukithiri kwa ujambazi, sasa imefika hatua ya kutisha zaidi! Mmesikia jinsi ambavyo majambazi walivyolipua garikwa bomu ikitokea maeneo ya Kilelema kuelekea Kasulu mjini!
Maisha yetu kila kona yapo mashakani. Kuanzia maeneo ya Mabamba, Kakonko, Manyovu na hadi ziwa Tanganyika! Wafanya biashara, watumishi wa serikali, na wafugaji, ndio wamekuwa wahanga wakubwa wa kadhia hii ya ujambazi.
Kila kukicha, utapata taarifa za utekaji wa wafanya biashara wakielekea sokoni na kwenye minada ya ng'ombe mipakani! Hapo, hupigwa na kunyang'anywa kila kitu wanachokuwa nacho. Pia, imefikia hatua, majambazi hayo huvamia vijiji usiku na kupita nyumba kwa nyumba za wafanyabiashara na watumishi wa umma kuwapora fedha na mali!
Naandika haya kwa uchungu mkubwa kwani nafahamu familia nyingi ambazo zimegeuka kuwa maskini kutokana na vitendo hivi! Mfano, ukienda vijiji vya Rumashi, Gwarama, Kabare, Muhange, Nyabibuye (Wilaya ya Kakonko), utapata simulizi za kutisha wanazopitia ndugu zetu huko! Ukienda maeneo ya Mabamba mpakani, watu wanalia! Ukienda mwambao mwa ziwa Tanganyika, wavuvi wananyang'anywa zana za uvuvi kila kukicha! Hali imekuwa tete kweli kweli! Tunaamini, kuwa majaambazi hao watakuwa wanapata ushirika wa raia wetu wasio waaminifu!
Chonde chonde serikali, tunaomba mshirikane na viongozi wa serikali za mitaa ili kubaini watu wanaoshirikiana na kuwapa taarifa majambazi hao juu ya safari za wafanya biashara na siku za mishahara kwa watumishi. Tunaoomba juhudi ziongezwe kwa kuwaska wote wanaoshiriki vitendo hivi viovu!!
Watu wa Kigoma wanastahili kuishi kwa utulivu ili waendelee na shughuli za maendeleo kama raia wengine!! Tumechoka kuishi kwa hofu kila kukicha.

Godfred Mbanyi, mbanyibg@yahoo.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments