Hivi tunapoamua kuoana huwa tunakurupuka au ndoa zimeishiwa baraka?
Tatizo lipo wapi nisaidieni waungwana
Mwanaume wa zamani alikuwa anaoa mwanamke hata hamjui na wakati mwingine hakuwahi hata kusalimia na ndoa zikadumu wengine mpaka wakazikana.
mwanaume wa leo unaoa mwanamke unamjua haswa tena wengine na watoto mmezaa wengine kuonyesha nyie wazinifu wa degree unamuoa wakati mja mzito, kwa fahari na mbwembwe muda si mrefu ndoa chaliii, nini shida?
mwanawake wa zamani pia alikuwa anaolewa na mwanaume ambaye hamjui hata na wakati mwingine hajawahi kukutana nae hata njiani lakini aliolewa na siku ya ndoa alikuwa na aibu machozi alilia kama anaenda chinjwa, ndoa zao zilidumu wengine mpaka wakazikana.
Haya nawe mdada wa leo unaolewa na mwanaume unamjua pengine mmmeishaishi na watoto au kitumbo ndii, siku ya ndoa wakavu na kwaito mnacheza na wakwe zenu nini tatizo?
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments