From: Masalu Mchembe <mchembemasalu@gmail.com>;
To: aron <aronmasalu@yahoo.com>;
Subject: Hello again
Sent: Sat, Aug 9, 2014 6:17:26 PM
Salaam Mh Nchemba naomba nikupongeze kwa kuona hali halisi ya watanzania na maisha yao. Mimi binafsi ni mwana ccm niseme wa kuzaliwa na kulelewa ktk chama,mara kadhaa nimekuwa nikisikitika sana pale ninapoona baadhi ya wana ccm wenzetu wanapotoa misimamo bila kuangalia hali halisi na nyakati. Mwl Nyerere aliangalia nyakati wakati wa Tanzania ama kufuata mfumo wa vyama vingi au kuendelea na mfumo wa chama kimoja. Nyerere, historia inaonyesha alikuwa mwangarifu sana ktk masuala mengi hususan yanayogusa taifa na ndiyo CHIMBUKO LA AMANI Tuliyonayo. Hali ya sasa ya utayarishaji wa katiba mpya, tulipofikia si pakuendelea kutumia maguvu , tukubali kusitisha turudi tujipange upya badala ya kuburuza na kutumia fedha ya watanzania kwa kitu ambacho hakina tija mbeleni. Wala tuache kufikiria kundi la wapinzani wetu kuwa ni dogo bila kuwafikiria watanzania wanaoweza kuwaunga mkono. Narudia tena kumkumbuka Nyerere aliwahi kusema 'jambo lolote linapotokea makundi matatu ya watu hujitokeza, kundi positive, negative na kundi neutral hili ni kubwa kuliko makundi yote na ni kundi hatari kwa vile ni rahisi kuvutiwa na kundi moja kati ya yale mawili. Shime nikupongeze tena. Kama ukawa wataendeleza msimamo wao kitu ambacho ni wazi; basi bunge lisitishwe. Asante samahani kwa kukupotezea muda wako. Aron masalu Geita |
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
Share this :
0 Comments