[wanabidii] MWENYEKITI JUKWAA LA KATIBA ATISHIWA KUUAWA

Thursday, July 31, 2014
MWENYEKITI wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba amejikuta akishikilia roho mkononi baada ya kupewa vitisho na mtu asiyejulikana kuwa atamuua bila kumueleza sababu.Image Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba.Taarifa kutoka chanzo chetu ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania zinasema kuwa, kiongozi huyo alipewa vitisho hivyo Julai 23, mwaka huu na kukimbilia Kituo cha Polisi Kijitonyama 'Mabatini' kutoa taarifa.

Uwazi lilimtafuta Kibamba kwa njia ya simu na kumuuliza kuhusu madai hayo ambapo alikiri."Ni kweli kabisa. Halafu kinachonishangaza ni kwamba, hii si mara ya kwanza kutishiwa, kikubwa ni kuhakikisha jeshi la polisi linaniwekea ulinzi wa kutosha lakini na mimi mwenyewe kuwa makini kwa kujihami."Mara ya kwanza ilikuwa kipindi kile cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni ni (Charles) Kenyela, nilitoa taarifa na kuimarishiwa ulinzi kwa viongozi wote wa Jukwaa la Katiba.

"Ukweli ni kwamba siogopi vitisho isipokuwa siwezi kudharau mambo ya namna hiyo, ndiyo maana natoa taarifa kwa usalama wangu," alisema Kibamba.Aliongeza kuwa, anachokiamini katika vitisho hivyo ni baada ya kutoa mapendekezo kuwa anataka katiba mpya iandikwe mwaka 2016 jambo ambalo anaamini watu ambao hawakuliunga mkono ndiyo wanaohusika kumtolea vitisho.Taarifa ya Kibamba kituoni hapo imepewa Kumbukumbu namba KJ/RB/6510/2014 KUTISHIWA KUUAWA KWA MANENO.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments